Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 09:03

Marekani haitosita kuzungumzia Uhuru wa watu wa Cuba

Rais Barack Obama akizungumza moja kwa moja kupitia video na Rais wa Cuba Raul Castro.
Rais Barack Obama akizungumza moja kwa moja kupitia video na Rais wa Cuba Raul Castro.

Katika mahojiano na ABC News, Rais Obama, amesema kwamba amemueleza Rais wa Cuba, Raul Castro, kwa njia ya simu kwamba Marekani itaendelea kuhamasisha demokrasia na kutetea haki za binadamu.

Rais Barak Obama, wa Marekani, amesema kwamba Marekani itaongea kwa ujasiri kuhusiana na uhuru wa watu wa Cuba.

Kauli hiyo imekuja baada ya kutangaza kurejesha uhusiano wa kawaida na kufungua ubalozi kwenye kisiwa hicho chenye utawala wa kikomunisti.

Katika mahojiano na ABC News, Rais Obama, amesema kwamba amemueleza Rais wa Cuba, Raul Castro, kwa njia ya simu kwamba Marekani itaendelea kuhamasisha demokrasia na kutetea haki za binadamu.

Ameendelea kusema kwamba hatarajii Rais Castro, kubadilisha Serikali yake mara moja, lakini mabadiliko ya vizazi yataimarisha urafiki katika siku za usoni.

Akitangaza makubaliano hayo awali huko White House, Rais Obama amesema ni wakati wa mtazamo mpya na Cuba, na kwamba miaka 50 ya kujitenga haijafaa chochote.

Wakati huo huo Rais Castro, alitoa tangazo lake kutoka mji mkuu Cuba, Havana, na kusema kuwa Rais Obama anastahili heshima na kutambuliwa na watu wa Cuba.

XS
SM
MD
LG