Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 15:50

Mapigano Sudan Kusini bado yanaendelea


Wanajeshi wa jeshi la serikali ya Sudan Kusini wakiwa Bentiu, huko Unity State, Sudan Kusini, Januari 12, 2014.
Wanajeshi wa jeshi la serikali ya Sudan Kusini wakiwa Bentiu, huko Unity State, Sudan Kusini, Januari 12, 2014.
Jeshi la Sudan Kusini lilipambana na waasi Jumatano huko kaskazini mwa eneo la jimbo la Upper Nile kufuatia wasi wasi wa kimataifa kwamba ghasia katika taifa hilo changa duniani zitaweza kugeuka na kuwa vita kamili vya wenyewe kwa wenyewe.

Msemaji wa serikali Philip Aguer aliiambia Sauti ya Amerika-VOA mapigano yanaendelea katika mji unaozalisha mafuta wa Malakal, mji mkuu wa jimbo la Upper Nile. Majeshi yanayomtii Rais Salva Kiir yanapigana na wanajeshi ambao wanamuunga mkono Makamu Rais wake wa zamani, Riek Machar ambaye alitolewa madarakani mwezi Julai.

Waasi walisema siku ya Jumanne kwamba waliukamata mji wa Malakal, dai ambalo serikali inalikanusha.

Madaktari wasio na mipaka wakitoa huduma
Madaktari wasio na mipaka wakitoa huduma

Madaktari wasio na mipaka wanasema mamia ya watu wamejeruhiwa katika muda wa siku chache zilizopita kutokana na mapigano katika majimbo ya Upper Nile, Unity na Jonglei.

Katika taarifa ya Jumatano kundi hilo la kutoa misaada lilisema liliwahudumia watu 116 wenye majeraha ya risasi huko Malakal na eneo la Nasir katika jimbo la Upper Nile.

Msemaji wa rais, Ateny Wek Ateny, Jumatano alitoa mwito wa umoja na alisema majeshi ya serikali yatashinda. Wawakilishi wa pande zote wamekuwa na mkutano nchini Ethiopia kwa mazungumzo ya uwezekano wa sitisho la mapigano.
XS
SM
MD
LG