Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 11:12

Wamalawi wasikitishwa na Banda kugomea kuapishwa kwa Mutharika


Rais mpya wa Malawi Arthur Peter Mutharika akitoa hotuba katika sherehe za kuapishwa kwake.
Rais mpya wa Malawi Arthur Peter Mutharika akitoa hotuba katika sherehe za kuapishwa kwake.
Kundi moja la kiraia na taasisi nyingi za kiraia nchini Malawi zimeeleza kusikitishwa kwao na hatua ya rais wa zamani wa nchi hiyo Joyce Banda kukataa kukabidhi madaraka rasmi kwa rais mpya Peter Muthariki.

Kundi la vyama vya kiraia Malawi linasema hatua ya Banda ilionyesha udhaifu wa uongozi baada ya rais huyo wa zamani kutohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Mutharika katika uwanja wa Blantyre Jumatatu. Rais Muthariki pia alionyeshwa kusikitishwa kwamba Banda hakutokea kumkabidhi rasmi uongozi wa taifa.

Katika hotuba yake ya kuapishwa Muthariki alisema " Nasikitika kwamba aliyenitangulia amekataa kuja hapa kunikabidhi madaraka....Nilikuwa nataka kushikana naye mkono na kusahau yaliyopita. Nimekuja na mkono wa amani. Naomba kila mtu aungane nami katika kuijenga upya Malawi."

Lakini msemaji wa Banda alisema kuwa rais huyo wa zamani hakuwajibika kikatiba kukabidhi madaraka kwa kiongozi mpya.

Tume ya Uchaguzi ya Malawi ilimtangaza Muthariki kuwa mshindi wa uchaguzi mkuu kwa asilimia 36 za kura huku chama cha rais Banda kikiwa kimepata asilimia 20 tu ya kura.
XS
SM
MD
LG