Jumatatu, Septemba 22, 2014 Local time: 06:10

Habari / Afrika

Makubaliano ya amani ya DRC yatiwa saini

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon asema makubaliano hayo ni chanzo cha maelewano ya kudumu baina ya serikali na makundi ya waasi.

 Rais wa DRC, Joseph Kabila
Rais wa DRC, Joseph Kabila
Baadhi ya viongozi wa kikanda  barani Afrika  wametia saini makubaliano yaliyodhaminiwa na Umoja wa Mataifa Jumapili, kwa lengo la kumaliza mtafaruku wa miongo miwili katika eneo la mashariki la Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Makubaliano hayo yametiwa saini  katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon alihudhuria sherehe hizo pia na kusema makubaliano hayo ni mwanzo wa  mchakato wa kufikia maelewano ya kudumu.

Inategemewa makubaliano hayo pia yatakuwa chanzo cha kuunda kikosi cha kikanda  kupambana na waasi katika eneo hilo lenye utajiri wa madini la DRC mashariki.

Viongozi hao wa Afrika walitegemewa kutia saini makubaliano hayo mwezi jana lakini yakaahirishwa baada ya kuibuka wasiwasi juu ya nani atakayeoongoza kikosi hicho cha kikanda.

Viongozi wa ukanda wa maziwa makuu  watakutana tena Kampala, Uganda Machi 15 kuendelea na majadiliano ya kusuluhisha mzozo baina ya serikali ya Kinshasa na kundi la waasi wa M23.
mjadala huu umefungwa
Maoni
     
There are no comments in this forum. Be first and add one

Mitaani

Your JavaScript is turned off or you have an old version of Adobe's Flash Player. Get the latest Flash player.
Maudhui ya wavuvi wa Bagamoyo-VOA Mitaanii
|| 0:00:00
...
 
🔇
X
20.09.2014 15:14
Wafanyabiashara wa samaki katika wilaya ya Bagamoyo, Tanzania waelezea changamoto zinazowakabili katika biashara kuu ya uvuvi, miongoni mwao ukosefu wa soko na mahala ya kuhifadhi samaki wanaovua.