Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 13:14

WHO inaeleza maji na mazingira safi yakosekana Afrika na Asia


Mwanamke mkimbizi wa Syria kutoka Kobani abeba majimkichwani katika kambi ya Suruc karibu na mpaka wa Uturuki na Syria
Mwanamke mkimbizi wa Syria kutoka Kobani abeba majimkichwani katika kambi ya Suruc karibu na mpaka wa Uturuki na Syria

Ripoti mpya imegundua kuwa mabilioni ya watu kote duniani bado wana upungufu wa mazingira safi na maji hasa katika maeneo ya vijijini ya kusini mwa jangwa la sahara barani Afrika na asia kusini mashariki. Ripoti ya shirika la Afya Duniani WHO, kwa niaba ya juhudi za idara mbali mbali za ndani zinazoitwa UN-Water, inasema ukosefu wa fedha unakwamisha maendeleo.

Ripoti hiyo imegundua kwamba theluthi mbili ya nchi 94 zilizofanyiwa utafiti zina sheria ambazo zinatambua kuwa maji ya kunywa na huduma za vyoo ni haki ya msingi ya binadamu kote ulimwenguni.

Zaidi ya asilimia 80 wana sera za kitaifa kuhusu maji ya kunywa na huduma za vyoo na Zaidi ya asilimia 75 zina sera za usafi.

Lakini sheria na nia nzuri wakati wote hazionyeshi matokeo yanayotakiwa. Ripoti inasema mafanikio yamepatikana katika kusambaza maji na huduma za vyoo kwa idadi kubwa ya watu.

Lakini inaelezea mwanya mkubwa katika ufadhili unakwamisha huduma kwa wanaume, wanawake na watoto bilioni 2.5 duniani kote katika kupata fursa ya huduma za msingi za usafi.

Inaeleza kuwa nyongeza ya watu milioni 748 hawana maji salama ya kunywa na mamilioni ya watu wanaishi bila maji safi na sabuni za kuosha mikono yao.

Mkurugenzi wa WHO katika idara ya afya ya umma, mazingira na afya ya jamii Maria Neira anasema ukosefu wa rasilimali hizi muhimu unachochea kuenea kwa magonjwa ya kuharisha na magonjwa mengine mengi yanatokanayo na maji machafu, kama vile kipindupindu, homa ya matumbo na homa ya manjano.

Dr.Neira anasema kila mtu anahitaji fursa ya usafi na maji salama lakini mazingira ya usafi yana utata.

XS
SM
MD
LG