Ijumaa, Mei 24, 2013 Local time: 05:15

Habari

Majeshi ya Syria yapiga wakazi wa Aleppo

UNHCR yasema idadi ya wakimbizi imeongezeka

Eneo la makazi nchini Syria
Eneo la makazi nchini Syria
ukubwa wa habari - +

Wanaharakati wa upinzani nchini Syria wameripoti mapigano makali kote nchini humo Jumanne yakiwemo mapigano katika mji mkubwa wa Aleppo. Kundi la kutetea haki za binadamu la Syria lenye makao yake Uingereza  limesema majeshi ya serikali yamepiga vitongoji vya mji wa Aleppo huku wakipambana vikali na waasi mjini humo. Taarifa za kundi hilo ambazo  hutegemea mashahidi zinasema majeshi ya rais Bashar al-Assad pia yameshambulia baadhi ya maeneo katika mkoa wa Deraa. Wanaharakati pia wanaripoti mapigano katika mji mkuu wa Damascus na katika mkoa  Homs.  Wakati huo, huo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ameleza hofu  yake  kufuatia mashambulizi makali ya majeshi ya Syria  dhidi ya raia.  Nalo shirika  wakimbizi la  Umoja wa Mataifa  UNHCR linaripoti kuwa idadi ya watu wanaotoroka  manyumbani mwao  kutoka mji wa Aleppo huko Syria inazidi kuongezeka. UNHCR inasema mapigano  baina ya majeshi ya serikali na waasi  yanahujumu juhudi za kuwasaidia  maelfu ya watu waliotoroka makwao. Shirika hilo linakisia hadi raia laki mbili wametoroka mji wa Aleppo na vitongoji vyake katika siku za karibuni.

mjadala huu umefungwa
Maoni
     
There are no comments in this forum. Be first and add one

Mitaani

Loading
12:00:00 / -:--:--