Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 01:41

Madaktari Tanzania warudi kazini


Madaktari Tanzania warudi kazini
Madaktari Tanzania warudi kazini

Madaktari waliokuwa kwenye mgomo hatimaye wameanza kurejea kazini, baada ya kufikia makubaliano na serikali.

Uwamuzi huo unafuatia mkutano kati ya madaktari na Waziri Mkuu siku ya Alhamisi na kukubaliana kwenye maeneo kadhaa ikiwemo suala la nyongeza ya posho, kuboresha mazingira ya kazi.

Bw. Haji Mponda waziri wa afya
Bw. Haji Mponda waziri wa afya

Akizungumza na Sauti ya Amerika Waziri wa Afya Haji Mponda anasema, madaktari walikubali kurudi nyumbani baada ya waziri mkuu kuahidi kutekeleza baadhi ya madai yao. "Miongoni mwa madai yao manane, tumechukuwa yaliyokuwa kama vipaumbele vyao na serikali kutekeleza ni suala la posho wakati wa masaa ya ziada, halafu masuala ya usafiri, na malazi".

Baada ya kugoma kwa karibu miezi mitatu, hatimaye nuru njema ilianza kuchomoza Ijumaa na tayari madaktari hao wameanza kutoa huduma ikiwemo kwenye hospitali ya taifa Muhimbili ambayo ililazimkika kufungwa kwa muda kutokana na mgomo huo.

Mwandishi wa Sauti ya Amerika aliyetembelea hospitali ya Muhimbili anasema kulikua na idadi ndogo ya wagonjwa na vitanda vingi vikiendelea kusalia vitupu. Wagonjwa wachache walilazwa kwenye hospitali hiyo wamesema angalau kwa leo wameanza kupata huduma.

Wakati huu madaktari bingwa pamoja na wale walioko kazini kwa mafunzo ya vitendo ambao ndiyo chimbuko kuu la mgomo huo wanatembelea katika wodi mbalimbali kwa ajili ya kukutana na wagonjwa.

Madaktari Tanzania warudi kazini
Madaktari Tanzania warudi kazini

Kulingana na afisa habari wa Hospitali hii ya taifa Muhimbili, Bwan Elimeli, hali ya wasiwasi iliyojotoeza hapo awali sasa imetoweka kabisa, na huduma zote zimeanza kutolewa.

Mwenyekiti wa Jumuia ya Madaktari tanzania, Dk.Ulimboka Stephen anasema madaktari wamerudi katika hospitali zote na majadiliano na serikali yanaendelea ili kuona ahadi zilizotolewa zinatekelezwa.

Katika hatua nyingine makundi ya harakati na kutetea haki za binadamu yametakwa kuwajibishwa kwa waziri wa afya na ustawi wa jamii pamoja na msidizi wake, kwa madai ya kuchochea mgogoro huo na kushindwa kutafuta ufumbuzi wa haraka.

Harold Sungusia anasema ingawa madaktari wamerudi kazini lakini tatizo kubwa lingali pale pale nalo ni ukosefu wa vifaa vya kufanya kazi, kwani anasema takwimu zinaonesha kuna mwanamke mmoja anaefariki Tanzania kwa saa moja kutokana na ukosefu wa vifaa vinavyostahiki.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha sheria na haki za binadamu Bi Hellen Kijibisamba, mamia ya watu wamepoteza maisha tangu kuanza kwa mzozo huo.

Wakati mgomo huu ukimalizika rasmi Ijuma, madhara yake yangali yakishuhudiwa na itachukua muda mrefu kwa sekta hiyo ya afya kutengamaa.

XS
SM
MD
LG