Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 23:55

Lowassa achukua fomu kuwania urais kupitia CHADEMA


Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania, Edward Lowassa
Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania, Edward Lowassa

Mbio za urais kuelekea uchaguzi mkuu mwezi Oktoba mwaka huu nchini Tanzania zimezidi kushika kasi ambapo Alhamis, Waziri Mkuu wa zamani bwana Edward Lowassa alichukua fomu rasmi ya kugombea nafasi ya urais kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA ambacho alijiunga nacho hivi karibuni baada ya kujitoa kutoka chama tawala cha CCM.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:30 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

CHADEMA mpaka Jumatano kilikuwa hakina mwanachama hata mmoja aliyechukua fomu ya kugombea urais ili kuungana na wagombea wengine waliopitishwa na vyama vingine vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi-UKAWA ambavyo tayari vina wagombea wa urais. Vyama hivyo ni Chama cha Wananchi-CUF na NCCR- MAGEUZI ambavyo kwa pamoja sasa wanatarajia kumtangaza mgombea mmoja ili kusimama kwa ajili ya kiti hicho cha urais.Chama kingine ndani ya UKAWA cha NLD hakijatoa mgombea wake wa urais.

Tundu Lissu akiongea na wafuasi wa chama chake.
Tundu Lissu akiongea na wafuasi wa chama chake.

Nderemo na vifijo zilitawala makao makuu ya CHADEMA jijini Dar Es Salaam ambapo mamia ya wapenzi na wanachama wa chama hicho walijitokeza kumsindikiza bwana Lowassa kuchukua fomu za kugombea kiti hicho kupitia chama chao.

Viongozi wengine wa CHADEMA akiwemo mwenyekiti Freeman Mbowe na mwanasheria wa chama hicho, Tundu Lissu walikuwepo kumsindikiza bwana Lowassa katika hatua hiyo ya kuchukua fomu.

Hata hivyo katika hafla hiyo ya kuchukua fomu ya kutaka kuingia Ikulu, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Willbroad Slaa hakuonekana kama ilivyokuwa siku ambayo bwana Lowassa alivyotangaza rasmi kujiunga na chama cha upinzani cha CHADEMA huku viongozi wa chama hicho wakisisitiza kwamba viongozi ambao hawakuwepo kwenye hafla hiyo wako kwenye majukumu mengine ya chama.

XS
SM
MD
LG