Ijumaa, Machi 27, 2015 Local time: 22:07

Habari / Muziki

Mwanamuziki wa Afrika Kusini awatumbwiza watu katika sherehe za kuapishwa Obama

Lira akiimba katika tamasha la kusherehekea kuapishwa kwa rais Obama
Lira akiimba katika tamasha la kusherehekea kuapishwa kwa rais Obama
Maelfu ya watu walimiminika katika jiji la Washington kuhudhuria kuapishwa kwa rais Barack Obama kwa mhula wa pili lakini zaidi pia walikuja kusherehekea katiaka tamasha mbali mbali zilizofanyika kote katika mji mkuu wa Marekani.

Miongoni mwa wasani mashuhuri wa Afrika alikuwepo  Lira kutoka Afrika Kusini. Aliimba katika sherehe za kwanza kuandaliwa ubalozi wa nchi mbali mbali za dunia ili kusherehekea pamoja na rais Obama na kusisitza umuhimu wa uhusiano wa kimataifa.

Ingawa rais hakuhudhuria tamasha hiyo Lira alimuimbia nyimbo maalum ambayo aliwahi kumuimbia rais wa zamani Nelson Mandela  wakati wa  kuadhimisha miaka 92 ya kuzaliwa kwake. “Something inside so strong.”
Lira mwimbaji chipikizi wa Afrika Kusinii
|| 0:00:00
...  
🔇
X
01.02.2013 21:45
Lira ni mwimbaji ambae alihudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Obama kwa mhula wa pili Januari 21 2013. Ni kijana mashuhuri wa Afrika Kusini ambae ameshapata tunzo kadhaa nchini mwake.


Lira anasema amefurahi kualikwa na kuhudhuria sherehe hizo ingawa hafahamu jinisi alivyoalikwa. “Mwanzoni mimi sikufahamu jinsi ilivyotokea. Tulipata barua pepe kueleza kwamba kuna tamasha inafanyika na wangelipenda tushiriki katika tamasha hilo. Basi mimi ninadhani ni jambo kubwa kuweza kuhudhuria na kuwepo hapa DC wakati wa sherehe za kuapishwa Obama.”

Baada ya kumsikiliza na sauti yake nyororo yakuvutia nimefahamu kwanini alialikwa. Akiwa na umri wa miaka 33 Lira ambae jina lake la kuzaliwa ni Lerato Molapo, ameshatoa albamu sita, nne akirikodi katika studio na mbili akiwa katika tamasha. Pamoja na dvd mbili, na ameshajinyakulia tunzo kadhaa nyumbani na kimataifa.

Lira anasema muziki wake ambao yeye huandika na kutunga mweneywe kwa lugha nne tofauti za Afrika Kusini pamoja na Kingereza na  Xosa  ni wa mtindo anoueleza ni Afro Soul.

“Kwa vile ni mtindo wa Soul zaidi, hata hivyo ninachanganya na Jazz na R&B kwa sababu hiyo ni midundo niliyokulia nayo. Na mdundo wa Afro bila shaka unatokana na asili yangu na lugha za kiafrika."

Anasifu muziki wake kutokana na kupenda na kusikiliza wanamuziki wa Marekani na wale si muziki wa magwiji na mdundo wa Afrika Kusini kama kina Hugh Masekela au Miriam Makeba.

“Muziki wa Afrika Kusini ulikuwa uempigwa marufuku nilipokuwa ninakuwa. Kwa hivyo sikuwa ninamsikiliza Miriam kwa mfano, hadi baadae kwa hivyo nyimbo nyingi tulokuwa tunasikiliza ni wa kina Stevie wonder, Aretha Franklin na wengine.”

Akiwa tayari ni mashuhuru huko Afrika Kusini Lira hivi sasa anasema yuko tayari kushuka kwenye jukwa la kimataifa. Tayari hapa marekani alishatembelea mwaka 2011 akifanya ziara ya majimbo matano mbele ya maelfu ya mashabiki. Anasema anawakilisha vijana wa afrika Kusini ambao wananufaika na mipaka iliyofunguliwa ambayo hapo awali ilikuwa imebanwa au kufungwa kabisa.

“Changamoto tuliyokuwa nayo katika kizazi hichi chetu , ambacho hivi sasa kiko huru, ni tufanyeje na uhuru huu wetu, Tufanye nini, inamaana gani kwangu mimi, kwangu mimi inamaana nina uhuru wa kufuata ndoto yangu nan a kuipanga ninapoendelea mbele. Hivi sasa kwa vile nimeshaikomboa afrika ninapanua nafasai zangu hivyo ndivyo ninavyo tumia uhuru wangu."
Lira akiimba mjini WashingtonLira akiimba mjini Washington
x
Lira akiimba mjini Washington
Lira akiimba mjini Washington


Akidhamiria kuendeleza utamaduni wake, Lira anasema kama wengine wa kizazi chake anajichukulia kama kiungo cha kuleta mabadiliko, kwa kuleta amani na umoja duniani kupitia muziki.

“Ninajitambulisha kama mwafrika wa mjini, yani tulicho nayo kama waafrika ni kwa sehemu tunaurithi wetu, lakini tunahamu pia kuwa walimwengu tughangiye katika utandawazi. Kile ninachona mimi ni kwamba imani ya kiafrika inaweza kuisaidia dunia ili kurudi katika imani ya kibinadamu yani Ubuntu kama tunavyiosema huko afrika kusini.”
Lira hivi sasa anatayarisha album mpya.
mjadala huu umefungwa
Maoni
     
There are no comments in this forum. Be first and add one
 • Jioni
  30 min

  Jioni

  Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa...

 • VOA Express
  30 min

  VOA Express

  VOA Express ni matangazo mapya yenye mwendo wa kasi yakiangalia habari mpya za...

 • Alfajiri
  30 min

  Alfajiri

  Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za...

 • Jioni
  30 min

  Jioni

  Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa...

Mitaani

Your JavaScript is turned off or you have an old version of Adobe's Flash Player. Get the latest Flash player.
Waandamana kupinga ubakaji Kenyai
|| 0:00:00
...  
🔇
X
27.03.2015 18:06
Mamia ya wanawake nchini Kenya hivi majuzi walishiriki maandamano kupinga vitendo vya ubakaji ambayo vimekithiri nchini humo