Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 09:07

Kundi la al-Shabab latishia kuuwa Wakenya


 Wanamgambo wa al-Shabab
Wanamgambo wa al-Shabab

Kundi la wanamgambo la al-Shabab kutoka Somalia linasema litauwa mateka wao kadhaa raia wa Kenya ikiwa Kenya haitatimiza madai yao ya kuwaachia waislam waliokamatwa kwa mashitaka ya ugaidi.

Kundi hilo lilitoa vitisho hivyo kwenye Video na kutumia mtandao wa Twitter Jumatano usiku . Video hiyo inaonyesha watu 6 wanaosadikiwa kuwa raia wa Kenya wakiwa wameshikiliwa na al-Shabab , wawili kwenye kamera na wanne kwenye picha.


Kwenye mtandao wa Twitter, al-Shabab wamesema watauwa watu hao ikiwa serikali ya Kenya haitatimiza madai yao ya kuwaachia huru waislam wote wanaoshikiliwa kwa mashitaka ya ugaidi nchini humo , na kuachiwa wengine waliopelekwa nchini Uganda kujibu mashitaka ya ugaidi nchini humo. Kundi hilo la wanamgambo linasema linaipa serikali ya Kenya hadi Februari 14 kujibu madai yake.
XS
SM
MD
LG