Ijumaa, Mei 24, 2013 Local time: 10:55

Habari

Kisimayo yaundiwa mkakati

wakuu wa jeshi wa nchi hizo wanasema watafanya mikutano kadhaa kabla ya kutekeleza majukumu ya kijeshi.

wapiganaji wa al- shabab
wapiganaji wa al- shabab
ukubwa wa habari - +
Mwai Gikonyo

Wakuu wa majeshi wa nchi za Afrika Mashariki na Sierra Leone wanakutana mjini Nairobi Kenya kujadili jinsi ya kuiteka bandari muhimu ya mji wa Kisimayo nchini Somalia inayodhibitiwa na wanamgambo wa Al Shabab.

Mkutano huu unashirikisha nchi zenye wanajeshi katika jeshi maalumu la muungano wa Afrika, Amisom lenye jukumu la kurejesha amani nchini Somali.

Ingawa hakuna taarifa yoyote iliyotolewa kuhusu kuvamia mji wa Kisimayo habari kutoka Nairobi zinasema wakuu hao wa majeshi watafanya mikutano kadhaa kabla ya kutekeleza jukumu lolote la kijeshi.

Mkutano huu unafanyika wakati umoja wa mataifa umetoa onyo la kuonya  nchi za Afrika kuhusu mpango wa kufanya mashambulizi katika nchi za Afrika hasa Kenya utakaotekelezwa na kundi hili la Al- Shabab.

mjadala huu umefungwa
Maoni
     
There are no comments in this forum. Be first and add one

Mitaani

Loading
12:00:00 / -:--:--