Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 10:19

Kikwete ahutubia bunge la Kenya


Rais Kikwete waTanzania
Rais Kikwete waTanzania

Rais Jayaka Kikwete wa Tanzania amehutubia mabaraza mawili ya Bunge la Kenya mjini Nairobi Jumanne alasiri na kusema uhusiano kati ya Kenya na Tanzania utaendelea kuimarika zaidi na uongozi ujao wa Tanzania.

Rais Kikwete aliwasili katika majengo ya bunge Nairobi mwendo wa saa tisa na dakika 40 na kulakiwa na kundi kubwa la wabunge na wanachama wa Baraza la Senate waliokuwa na hamu ya kumsikiliza kiongozi huyo wa Tanzania anayetarajiwa kustaafu kwenye uongozi baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu nchini Tanzania tarehe 25 mwezi huu.

Kikwete ahutubia bunge la Kenya
please wait

No media source currently available

0:00 0:03:00 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Kulikuwa na ulinzi mkali katika majengo ya bunge na wabunge wa chama tawala na wale wa upinzani walimiminika kwa wingi ndani ya majengo ya Bunge.

Baadaye Rais Kikwete aliwahutubia wabunge na kusema ni siku 19 kabla ya uchaguzi mkuu Tanzania na alialikwa na Rais Kenyatta kufika Kenya kuwaaga raia wa Kenya. Amesema Kenya ni rafiki na mshiriki mkubwa wa Tanzania. Amesema baada ya mkasa na ghasia za uchaguzi mkuu wa mwaka 2007 nchini Kenya alifika mara moja hapa Nairobi kutatua mzozo huo bila kualikwa isipokuwa kwa yeye mwenyewe kuomba kwenda Kenya kusaidia kupata ufumbuzi.

Ziara ya Rais Kikwete hapa Nairobi imekuwa na shughuli nyingi. Gavana wa jiji kuu la Nairobi Evans Kidero amemtunukia Rais Kikwete heshima kuu kwa kumkabidhi ufunguo maalum kama ishara ya mtu huru mjini Nairobi. Pia barabara mashuhuri ya Milimani imebadilishwa jina na kupewa jina la Jakaya Kikwete Road.

XS
SM
MD
LG