Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 15:22

Kiir akubali kutia saini mkataba wa amani wa Sudan Kusini


Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir (L) na Makamu Rais wa zamani ambaye amekuwa kiongozi wa waasi Riek Machar, huko Addis Ababa
Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir (L) na Makamu Rais wa zamani ambaye amekuwa kiongozi wa waasi Riek Machar, huko Addis Ababa

Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir amekubali kutia saini makubaliano ya amani yanayolenga kumaliza miezi 20 ya vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini mwake.

Katika barua iliyoifikia program ya Sauti ya Amerika-VOA ya South Sudan In Focus, taasisi ya kieneo IGAD inayoundwa na mataifa ya Afrika mashariki inasema mkataba unatarajiwa kutiwa saini hapo Jumatano huko Juba, mji mkuu wa Sudan Kusini.

Taasisi ya IGAD katika mkutano huko Addis Ababa
Taasisi ya IGAD katika mkutano huko Addis Ababa

IGAD imekuwa mpatanishi wa mazungumzo ya kumaliza vita kati ya serikali ya bwana Kiir na waasi wanaoongozwa na Makamu Rais wake wa zamani, Riek Machar. Bwana Machar alitia saini mkataba huo mjini Addis Ababa hapo Agosti 17 lakini Rais wa Sudan Kusini alikataa akisema kwamba amani kwa mujibu wa mkataba haiwezi kuendelezwa.

XS
SM
MD
LG