Ijumaa, Machi 27, 2015 Local time: 02:44

Habari / Marekani

Kerry aidhinishwa kuwa waziri wa mambo ya nje

Seneta John Kerry baada ya kuidhinishwa kuwa mwanadiplomasia wa juu wa Marekani Januari 29, 2013.
Seneta John Kerry baada ya kuidhinishwa kuwa mwanadiplomasia wa juu wa Marekani Januari 29, 2013.
Baraza la Senate  la Marekani limemwidhinisha Seneta John Kerry kuwa waziri wa mambo ya nje kwa kura 93 dhidi ya 3. Kerry ataondoka kwenye wadhifa wake kama seneta wa jimbo la Massachusetts na kuchukua  nafasi ya Hillary Clinton kama mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa serikali ya Rais Barack Obama kwa dunia.

Kuidhinishwa kwa bw. Kerry kama waziri wa mambo ya nje wa Marekani hakukuwa na shaka. Maseneta wa vyama vyote viwili  walimpongeza kabla ya kura hiyo kupigwa Jumanne. Mdemokrat Ben Cardin alielezea wasifu wa Kerry katika  kamati ya baraza la senate juu ya maswala ya nje.“Sidhani kuna mtu katika baraza hili aliyehudumu kwa muda mrefu, kusafiri katika maeneo mengi na kukutana na watu  akiwakilisha taifa letu katika ngazi ya kimataifa kama yeye.”

 Naye seneta Bob Corker wa chama cha Republican alikuwa na maoni sawa na hayo. “Sijui mtu yeyote aliyeishi maisha yake na kujua mengi kuhusu  kazi za wizara ya mambo ya nje kama seneta John Kerry.”

Maseneta walikiri kuwa bw. Kerry alijitosa mwenyewe katika maswala ya kimataifa mapema katika maisha yake. Akiwa kijana alipigana katika vita vya Vietnam na baadaye kukemea ukatili alioshuhudia. Kama mbunge, Kerry amesafiri sana katika nchi za nje kwa zaidi ya miongo miwili.

Seneta  mdemokrat Robert Menendez ambaye atachukua wadhifa wa Kerry kama mwenyekiti wa kamati ya senate juu ya maswala ya nje, alielezea orodha ndefu ya mafanikio ya bw. Kerry. “Amekuwa mtetezi wa program zinazozuia  silaha za nuklia na kibaolojia kufikia mikono ya nchi  hatari na magaidi. Alikuwa mtetezi mkuu wa amani kati ya Sudan na  Sudan kusini na kutekeleza wajibu muhimu katika kura ya maoni ya mwaka wa 2011. Anafahamika vyema kama mbunge anyefanya kazi na vyama vyote viwili vya kisiasa Marekani.”

Wachambuzi wanasema imani  ya Seneta Kerry kuhusu wajibu wa Marekani duniani na matumizi salama ya nguvu zake za kijeshi yanawiana na yale ya  rais  Barack Obama.
mjadala huu umefungwa
Maoni
     
There are no comments in this forum. Be first and add one
 • Jioni
  30 min

  Jioni

  Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa...

 • VOA Express
  30 min

  VOA Express

  VOA Express ni matangazo mapya yenye mwendo wa kasi yakiangalia habari mpya za...

 • Alfajiri
  30 min

  Alfajiri

  Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za...

Mitaani

Your JavaScript is turned off or you have an old version of Adobe's Flash Player. Get the latest Flash player.
Ajali barabarani Tanzania zaongezekai
|| 0:00:00
...  
🔇
X
18.03.2015 16:17
Matukio ya ajali mbaya za barabarani Tanzania hivi karibuni zinasemekana kuwa ishara ya ongezeko la uzembe na kutozingatia sheria za usalama barabarani, kulingana na watalaam.