Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 12:21

Kenya yapinga ripoti ya al-Jazeera


Mashambulizi ya Westgate Mall, Nairobi Septemba, 2013
Mashambulizi ya Westgate Mall, Nairobi Septemba, 2013

Kenya ilisema walioandaa program hiyo kamwe hawakutilia maanani maisha ya Wakenya wengi wasio na hatia waliouawa na magaidi.

Serikali ya Kenya imesema inaweza kuwashitaki waliotengeneza kipindi cha televisheni kinachoshtumu Kenya kwa kutumia vitengo vya mauaji katika jeshi lake la polisi, kuuwa waislamu wenye msimamo mkali. Kituo hicho cha televisheni chenye makao yake makuu nchini Qatar kilipeperusha hewani program hiyo Jumatatu.

Katika mfululizo wa jumbe za Twitter na taarifa rasmi zilizotolewa Jumanne, maafisa wa Kenya walikanusha vikali matumizi ya vitengo vyovyote vya mauaji katika idara yake ya polisi.

Serikali hiyo pia imegiza uchunguzi kamili ufanywe ili iweze kuwashtaki wahusika waliohojiwa kwenye kipindi hicho cha televisheni.Program ya al- Jazeera ilionyesha mahojiano na wanaume waliosema walikuwa maafisa wa kitengo cha mauaji cha polisi wa Kenya wakikiri kushiriki katika mauaji ya kihohela.

Wanaume hao waliogubika nyuso zao wakati wa mahojiano hayo walisema walitekeleza mauaji hayo kufuatia amri ya maafisa wa juu katika serikali ya Kenya.

Serikali ya Kenya imesema program hiyo iliandaliwa maksudi kutoa taarifa za uwongo,ili kuchochea ghasia na jazba kwa wanamgambo wa Kiislam na wafuasi wao dhidi ya taifa hilo la Afrika Mashariki. Ilisema walioandaa program hiyo kamwe hawakutilia maanani maisha ya Wakenya wengi wasio na hatia, waliouawa na magaidi.

Kundi la wanamgambo wa Somalia al-Shabab limefanya mashambulizi kadhaa dhidi ya Kenya, tangu serikali hiyo ilipopeleka majeshi yake Somalia kupigana na wanamgambo hao miaka mitatu iliyopita.

Shambulizi kubwa lililofanywa na al-Shabab nchini humo ni lile la maduka ya kifahari ya Westgate Mall jijini Nairobi mwaka 2013 ambapo watu 70 waliuawa.

XS
SM
MD
LG