Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 10:52

Kenya yadai fidia kwa mahujaji waliokufa Mecca


Mahujaji wakisaidiwa baada ya mkanyagano
Mahujaji wakisaidiwa baada ya mkanyagano

Baraza Kuu la Waislamu nchini Kenya SUPKEM limeitaka serikali ya Saudi Arabia kulipa fidia kwa mahujaji 6 kutoka Kenya waliokufa kwenye mkasa uliotokea wiki iliyopita Mecca, Saudi Arabia. Wengine 9 wamepotelea nchini Saudi Arabia.

Akizungumza na waandishi wa habari hapa mjini Nairobi, mwenyekiti wa kitaifa wa Supkem, Abdulghafur El Busaidy, amesema serikali ya Saudi Arabia inafaa kuwalipa fidia mahujaji 6 kutoka Kenya waliokufa kwenye ule mkanyangano wa mahujaji wiki iliyopita. Alisema kufikia sasa mahujaji wengine 9 kutoka Kenya hawajulikani waliko kufuatia mkasa huo.

Kenya yadai fidia ya mahujaji
please wait

No media source currently available

0:00 0:03:33 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Tanzania ilipoteza mahujaji 6 na wengine 50 hawajulikani walipo.

Baraza hilo linasema mahujaji waliokufa kutoka Kenya tayari wamezikwa nchini Saudi Arabia kuambatana na utaratibu wa dini ya kiislamu.

Mwenyekiti huyo Supkem anasema mahujaji wengi wanakuwa na matumaini na matarajio makubwa kabwa kabla ya kuondoka hapa nchini. Lakini yaliyotokea ni majaliwa ya mungu na kilichosalia hivi sasa ni kwa serikali ya Saudia ilipe fidia kwa jamaa ya mahujaji waliokufa kama ilivyofanya kwa wale walio-angukiwa na winchi siku kumi kabla ya hijja kuanza.

Baraza hilo la waislamu nchini Kenya linasema jamaa za mahujaji waliokufa tayari wamejulishwa kuhusu mkasa huo. Kwa jumla zaidi ya mahujaji 1,100 walipoteza maisha yao wakati wa mkasa huo. Baadhi ya mahujaji elfu 4 kutoka Kenya sasa wameanza kurejea nyumbani. Imeripotiwa na Mwai Gikonyo, Nairobi.

XS
SM
MD
LG