Jumapili, Februari 14, 2016 Local time: 04:38

  Makala Maalum / Uchaguzi Kenya 2013

  Katiba mpya ya Kenya na uchaguzi wa Machi 4

  Mshindi wa kiti cha rais ataapishwa rasmi Machi 26. Lakini kukiwa na uchaguzi wa marudio, ataapishwa Aprili 30.

  Rais Mwai Kibaki (R) akisajiliwa kupiga kura Novemba 19, 2012, kwa uchaguzi mkuu Machi 4, 3013.
  Rais Mwai Kibaki (R) akisajiliwa kupiga kura Novemba 19, 2012, kwa uchaguzi mkuu Machi 4, 3013.
  Esther Githui-Ewart
  Katika mfululizo wa makala zetu juu ya uchaguzi mkuu nchini Kenya,tunamulika katiba mpya ya Kenya na namna ilivyobadilisha utaratibu wa uchaguzi ujao, ikilinganishwa na chaguzi za hapo nyuma.

  Moja ya nguzo kuu za mabadiliko ya kisiasa nchini Kenya ni katiba mpya iliyoidhinishwa rasmi Agosti 27 mwaka wa 2010. Na  tangu hapo  unapozungumza na wakenya mara kwa mara utawasikia wakielezea haki zao na kunukulu katiba  yao mpya kwa majivuno..kwamba hili na hili limewezekana kutokana na katiba mpya.

  Katiba mpya ya Kenya ni matokeo ya juhudi za wakenya, waliotumia muda wao mwingi kutoa maoni  katika rasimu ambayo hatimaye ilipigiwa kura, kukubalika na kuandikwa na wataalam.

  Mojawapo ya mabadiliko makubwa katika siasa za Kenya yaliyotokana na katiba hiyo ni utaratibu wa uchaguzi mkuu. Hapo awali uchaguzi huo ulihusu rais na wabunge. Lakini ifikapo Machi 4, wakenya watachagua wawakilishi sita. Kuna rais, wabunge, magavana, maseneta  na wengine wengi.
   
  Patrick Ochieng ni mkereketwa wa haki na demokrasia nchini Kenya na pia mkurugenzi mtendaji wa shirika la kitaifa la Ujamaa. Anasema ,katiba imeleta utaratibu mpya kwenye uongozi na kwenye uchaguzi.”  Kutokana na mabadiliko hayo kutakuwa na serikali kuu, na pia serikali ya ugatuzi na uwakilishi kwenye mabaraza 47 ya Kenya. 

  Ripoti juu ya katiba
  Ripoti juu ya katibai
  || 0:00:00
  ...    
   
  X


  Msukumo wa kutaka mabadiliko ya kikatiba una chanzo chake au shinikizo kutoka  siasa za mashinani au  siasa za kitaifa na hata kimataifa Ifahamike kuwa wakenya walichoshwa na katiba ya zamani iliyompa mamlaka makuu rais wa nchi.

  Uchaguzi wa Machi nne mwaka huu utaongeza  idadi ya viongozi wa kisiasa nchini Kenya kutoka viti 222 hadi 290 na ujenzi wa  kisasa wa kupanua bunge unaendelea.Katiba hiyo mpya pia inaelezea bayana majukumu katika kila ngazi ya uwakilishi.

  Lakini  kwa sasa wagombea viti wamo mbioni katika kampeni za mwisho, mwisho. Na imewalazimu mahasidi wa zamani wa kisiasa kuunda ushirika na miungano ya vyama ili kushinda uchaguzi huu .Mkurugenzi mtendaji wa shirika  la Ujamaa Patrick Ochieng anasema  hilo pia limesukumwa na katiba mpya ya Kenya:

  Kwa hiyo kwa mpiga kura wa Kenya, katiba inamlazimu kuwachagua wawakilishi sita, miongoni mwao rais, seneta, mbunge, gavana na wengine. Atakayechaguliwa kuwa rais  mpya wa Kenya  sharti apate asili mia 51 ya kura zilizopigwa, pamoja na asili mia 25 za kura kwenye nusu ya mabaraza 47 ya taifa hilo.
   
  Ikiwa mshindi atabainika  wazi bila mashaka yoyote  katika duru ya kwanza ya uchaguzi,  rais huyo mteule ataapishwa Machi 26 mwaka huu. Lakini ikiwa kutakuwa na uchaguzi wa marudio, rais ajaye wa Kenya ataapishwa Aprili 30. Kwa sasa maamuzi ya nani ataunda serikali ijayo ya Kenya imo mikononi mwa wapiga kura.
  mjadala huu umefungwa
  Maoni
       
  Hakuna mtu ameandika maoni hapa. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.