Ijumaa, Mei 22, 2015 Local time: 11:27

Habari / Afrika

Kampuni za simu Uganda kuadhibiwa kwa huduma mbaya

Simu ya mknoni ya mtindo wa zamani
Simu ya mknoni ya mtindo wa zamani
Tume ya mawasiliano nchini Uganda imetangaza kuwa itaanza kuziadhibu kampuni zote za simu nchini Uganda kwa sababu zinatoa huduma duni za simu. Haya yalitamkwa na mkuu wa tume ya mawasiliano Godfrey Mutabazi, Jumanne wakati akizungumza na waandishi habari mjini Kampala kuhusu matokeo ya utafiti wa kiwango cha huduma kinachotolewa na kampuni za simu.

Na Leyla Ndinda, Kampala
Na Leyla Ndinda, Kampalai
|| 0:00:00
...    
🔇
X

Uganda ikiwa na wananchi milioni 33, kwa kujibu wa tume ya mawasiliano nchini humo, watu milioni 16 wanatumia simu za mikononi.
 
Kampuni nane za simu zimesajiliwa kutoa huduma za simu. Ripoti iliyochapishwa na tume ya mawasiliano Uganda baada ya kufanya utafiti wa miezi minne kuanzia mwezi Julai hadi mwezi Oktoba mwaka jana inaonyesha kuwa kampuni hizi zinakiuka sheria zilizowekewa na tume hii.

Kwa mfano idadi ya simu ambazo zinakatika ovyo wakati wa mawasiliano ni zaidi ya kiwango kinachokubaliwa cha asilimia mbili, wateja wanatumiwa ujumbe mfupi wa matangazo kutoka kwa kampuni za simu na kukatwa pesa ilhali hawajaomba kupokea matangazo haya pamoja na mfumo mbaya wa simu unavyosababisha mawasiliano kuwa magumu.

Mkuu wa tume ya mawasiliano nchini Uganda Godfrey Mutabazi anasema “tutafanya ukaguzi wa kampuni hizi siku thelathini zijazo. Ikiwa wataendelea kuwanyanyasa wateja basi wataadhibiwa. Tutakuwa tunawatoza asilimia fulani ya pesa kutoka kwa mapato yao.

Huduma wanazotoa ni duni sana na ni jambo la kuaibisha sana kuwa kampuni hizi zinaendelea kukiuka onyo la tume ya mawasiliano. Kilichosalia sasa ni kuwaadhibu na ikiwa wataendelea kuwatolea wananchi huduma duni  basi tutairejelea sheria na huenda tukazitupilia mbali leseni zao”.

Tume ya mawasiliano pia inaonya dhidi ya kampuni za simu kupunguza sana kiwango cha pesa wanazotoza kwa kila dakika moja ya mawasiliano na pia pesa wanazotoza kwa kila ujumbe mfupi unaotumwa. Hii ni kwa sababu ikiwa mapato yao ni ya chini sana  basi huduma watakayotoa nayo pia itakuwa mbaya.
mjadala huu umefungwa
Maoni
     
There are no comments in this forum. Be first and add one
 • Alfajiri
  30 min

  Alfajiri

  Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za...

 • Jioni
  30 min

  Jioni

  Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa...

 • VOA Express
  30 min

  VOA Express

  VOA Express ni matangazo mapya yenye mwendo wa kasi yakiangalia habari mpya za...

 • Alfajiri
  30 min

  Alfajiri

  Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za...

Mitaani

Your JavaScript is turned off or you have an old version of Adobe's Flash Player. Get the latest Flash player.
Matatizo ya Miundombinu Dar Es Salaami
|| 0:00:00
...  
🔇
X
21.05.2015 05:17
Wakazi wa Dar es Salaam wanasema ukosefu wa miundo mbinu inayostahiki ndiyo inasababisha matatizo ya uchafu, huduma za maji na nishati.