Jumanne, Machi 03, 2015 Local time: 21:44

Habari / Afrika

Kabila akabiliwa na upinzani kuzungumza na M23.

Wapiganaji wa M23 wawasili Goma
Wapiganaji wa M23 wawasili Goma
Serikali ya Rais Joseph Kabila imetangaza mpango wa kuanza mazungumzo na waasi wa kundi la M23 ili kutafakari na kukagua mkataba wa amani wa Marchi 2009  baina ya Serikali na waasi.

Mkutano huo utakaofanyika mjini Kampala unatarajiwa kuhudhuriwa na wajumbe wa serikali, waasi wa M23 pamoja na wajumbe wa mashirika ya kiraia. Hata hivyo ajenda  rasmi ya mkutano huo bado haijatangazwa.

Kwa siku mbili mfululizo Rais Kabila amekuwa akikutana na baadhi ya viongozi wa idara za serikali na wabunge ilikuwapa mtizamo wake kuhusu vita vya Kivu.

UDPS yapinga mazungumzo na M23 120412
UDPS yapinga mazungumzo na M23 120412i
|| 0:00:00
...    
🔇
X

Aubin Minaku, Spika wa bunge la DRC na mshirika wa karibu wa Rais Kabila, akizungumza na vyombo vya habari amesema kwamba mkutano huo wa Kampala unalenga kutafakari juu ya  malalamiko ya waasi wa M23.

Kauli hiyo ya spika wa bunge imefuatia ombi la waasi wa M23 la kutaka upinzani wa kisiasa, mashirika ya kiraia na wakongomani wanaoishi nje ya nchi kushirikishwa kwenye mazungumzo. Spika wa bunge la DRC amesema kwamba siyo vibaya kuweko na watu wa tabaka zote za taifa kushirikishwa kwenye mazungumzo.

Suala la kuwepo kwa mazungumzo na waasi limezusha utata mkubwa huko kinshasa ambapo vyama vikuu vya upinzani vinapinga mazunguzmo hayo. Msemaji wa chama kikuu cha upinzani UDPS, Augustin Kabuya ameiambia VOA kwamba hawatoshiriki katika aina yeyote ile ya mazungumzo baina ya serikali na waasi wa M23.

UDPS inaeleza kwamba serikali ya Kabila, si halali sawa na vile waasi wa M23, na kuwataka waasi hao kutotumia  jina la kiongozi wao, Etienne Tshisekedi katika kutetea vita vyao, kwa sababu UDPS haiwezi kamwe kutumia silaha ilikuchukuwa madaraka.

Lakini kwa upande wake chama cha UNC cha Vital Kamerhe kimesema kwamba kiko tayari kuhudhuria mazungumzo ya Kampala ikiwa kitaalikwa.

Msemaji wa tawi la kisiasa wa kundi la M23 Bertrand Bisimwa ambaye ameiambia VOA kwa njia ya simu kwamba wamepokea mualiko wa kwenda Kampala kwa ajili ya mazungumzo, amesisitiza kwamba ajenda ya mkutano huo ni lazima iwape nafasi  wapinzani na mashirika ya kiraia kuhudhuria  mkutano huo.

Makundi mengine ya wapiganaji pia yameelezea nia yao ya kutaka yashirikishwe kwenye mazungumzo sawa na M23.
mjadala huu umefungwa
Maoni
     
There are no comments in this forum. Be first and add one
 • Jioni
  30 min

  Jioni

  Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa...

 • VOA Express
  30 min

  VOA Express

  VOA Express ni matangazo mapya yenye mwendo wa kasi yakiangalia habari mpya za...

 • Alfajiri
  30 min

  Alfajiri

  Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za...

Mitaani

Your JavaScript is turned off or you have an old version of Adobe's Flash Player. Get the latest Flash player.
Wakenya watoa maoni kuhusu mfumo wa dijitalii
|| 0:00:00
...  
🔇
X
26.02.2015 19:55
Tangu uamuzi wa serikali kuondoa matangazo ya analog Wakenya wamekuwa na maoni tofauti kuhusu mfumo huo na kuzimwa kwa baadhi ya matangazo ya mashirika makuu ya televisheni Kenya