Jumatano, Oktoba 01, 2014 Local time: 16:15

Habari / Afrika

John Kerry ateuliwa kuchukua nafasi ya Clinton

Seneta John Kerry ambaye anatarajiwa  kuchukua nafasi ya Hillary Clinton wote kutoka chama cha Democrat
Seneta John Kerry ambaye anatarajiwa kuchukua nafasi ya Hillary Clinton wote kutoka chama cha Democrat
Maafisa waandamizi wa Marekani wanasema Rais Barack Obama atamteuwa seneta John Kerry kuchukua nafasi ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani.

Maafisa wa utawala wanasema bwana Obama atatangaza rasmi uteuzi huo baadae  Ijumaa.

Kerry, m-Democrat kutoka jimbo la kaskazini mashariki la  Massachusetts amehudumu kama mwenyekiti wa kamati ya seneti inayoshughulika na uhusiano wa nje na amesafiri  kwenda sehemu mbali  kwa niaba ya Rais Obama kujadili masuala muhimu duniani kote kutoka Afrika hadi Pakistan. Pia anatambulika kama mkongwe wa vita vya Vietnam.

Kerry mwenye umri wa miaka 69 aliwahi kuwania nafasi ya urais katika chama cha Democrat mwaka 2004 na kushindwa kinyang’anyiro hicho na Rais  aliyekuwa madarakani wakati huo George W.Bush.Kama akipitishwa na seneti, Kerry atachukua nafasi ya hivi sasa ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Hillary Clinton ambaye alitangaza hana mpango wa kuendelea katika wadhifa huo katika muhula wa pili wa utawala wa Obama.
mjadala huu umefungwa
Maoni
     
There are no comments in this forum. Be first and add one

Mitaani

Your JavaScript is turned off or you have an old version of Adobe's Flash Player. Get the latest Flash player.
Maudhui ya wavuvi wa Bagamoyo-VOA Mitaanii
|| 0:00:00
...
 
🔇
X
20.09.2014 15:14
Wafanyabiashara wa samaki katika wilaya ya Bagamoyo, Tanzania waelezea changamoto zinazowakabili katika biashara kuu ya uvuvi, miongoni mwao ukosefu wa soko na mahala ya kuhifadhi samaki wanaovua.