Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 05:49

Waziri wa Marekani John Kerry akutana na mwenzake wa Cuba.


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry, akisalimiana na mwenzake wa Cuba, Bruno Rodriguez mjini Washington, Jumatatu.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry, akisalimiana na mwenzake wa Cuba, Bruno Rodriguez mjini Washington, Jumatatu.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry alisema kurejeshwa mahusiano ya kidiplomasia na Cuba ni mwanzo mpya lakini alisema tofauti nyingi bado zipo baina ya mataifa hayo mawili na kuonya kwamba mchakato wa kurejesha uhusiano wa kawaida utachukua muda mrefu.

Haya ameyasema Jumatatu saa kadhaa baada ya sherehe kufanyika Havana na Washington kuadhimisha kurejeshwa kwa uhusiano baada ya zaidi ya miongo mitano ya uhasama.

Kerry alisema maslahi ya nchi zote mbili yatalindwa vyema kwa ushirikiano wala sio utengano. Baada ya mkutano na Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba, Bruno Rodriguez Parrilla alifanya ziara ya kwanza kwenye wizara ya mambo ya nje ya Marekani, kuwahi kufanywa na Waziri wa Mambo ya Nje tangu mwaka 1958.

Sherehe za kurejesha tena uhusiano wa kidiplomasia huko Havana, July 20, 2015.
Sherehe za kurejesha tena uhusiano wa kidiplomasia huko Havana, July 20, 2015.

Parrilla alisema mkutano wake na Kerry Jumatatu ulikuwa wa mafanikio, lakini amesisitiza bado kuna tofauti kadhaa zilizoko baina ya nchi hizo mbili. Ametoa wito wa kuondolewa kwa vikwazo vya kiuchumi vya Marekani dhidi ya Cuba na kusihi kurejeshwa haraka kwa eneo linalotumiwa na Marekani kama kituo cha jeshi huko Guantanamo Bay.

Sherehe za ufunguzi wa ubalozi wa Marekani nchini Cuba zitacheleweshwa hadi pale bwana Kerry atakapo safari kwenda Havana, lakini ubalozi utafanya kazi kama kawaida kuanzia sasa. Kerry alitangaza Jumatatu kuwa atasafiri kwenda Havana Agosti 14.

Mabadiliko haya ya kihistoria yamekuja baada ya miaka 54 ya kuvunjika kwa uhusiano wa kidiplomasia ambao ulitokea wakati wa utawala wa Rais wa Marekani, John Kennedy

XS
SM
MD
LG