Jumapili, Mei 19, 2013 Local time: 06:20

Habari

John Dramani Mahama achukua madaraka Ghana.

Makamu rais wa Ghana John Dramani Mahama atamalizia muhula wa rais John Atta Mills .

Makamu rais wa Ghana John Mahama akiapishwa kuchukua madaraka.
Makamu rais wa Ghana John Mahama akiapishwa kuchukua madaraka.
ukubwa wa habari - +

Makamu rais wa Ghana John Dramani Mahama atamalizia muhula wa rais John Atta Mills ambaye alifariki ghafla Jumanne. Mahama aliapishwa kuchukua madaraka saa kadhaa baada ya maafisa kutangaza kifo cha Bw. Mills.

Ghana inatarajiwa kufanya uchaguzi ifikapo Desemba. Mchambuzi wa kisiasa Emmanuel Akwetey, mkurugenzi wa taasisi ya utawala wa kidemokrasia  aliiambia VOA kwamba anatarajia chama tawala cha Democratic Congress kumtangaza Bw.Mahama kama mgombea wake. Alisema kwamba Bw.Mahama alifanya kampeni na hayati  rais na kwamba muda uliobaki kabla ya upigaji kura ni mfupi.

Amesema chama cha upinzani cha New Patriotic Party kimesitisha kampeni zake kwa heshuima ya Bw. Mills na kusaidia kuunganisha nchi.

 

 

mjadala huu umefungwa
Maoni
     
There are no comments in this forum. Be first and add one

Mitaani

Loading
12:00:00 / -:--:--