Jumamosi, Mei 30, 2015 Local time: 19:22

Habari / Afrika

Jeshi la Congo lakamata watu kadhaa kwa shutuma za ubakaji

Wanajeshi wa jeshi la Congo wakiwa kwenye mji wa Goma, DRC, December 3, 2012.
Wanajeshi wa jeshi la Congo wakiwa kwenye mji wa Goma, DRC, December 3, 2012.
Waathirika wa ubakaji wasiopungua 70 wamekuwa wakipata matibabu katika kijiji kidogo cha Minova huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC ambacho karibuni kilivamiwa na watu waliovalia sare za jeshi, kwa mujibu wa Umoja wa mataifa. Jeshi la DRC lina kituo kikubwa huko Minova na linasema limewakamata wanajeshi kadhaa huko walioshukiwa kwa ubakaji na wizi wa ngawira.
 
Mji wa Minova upo katika jimbo la Kivu Kusini ni mahali ambapo makundi ya jeshi la Congo yalijikusanya tena baada ya kushindwa na waasi wa M23 katika mapigano yaliyotokea mwezi uliopita huko Goma.

Hali ya usalama huko Minova ilikuwa mbaya mwishoni mwa mwezi uliopita na iliripotiwa kwamba wanajeshi walilikimbia eneo na walifanya wizi wa ngawira wakati wanavuka katika mji huo.

Umoja wa Mataifa unasema waathirika wa ubakaji huwenda wametokea umbali kadhaa kutoka mji huo na huku washutumiwa wakuu ni wanajeshi wanaume wanaweza kuwa wanatoka makundi mbali mbali.

Kamanda mpya wa majeshi ya nchi kavu ya DRC, Jenerali Francois Olenga, aliitisha mkutano wa maafisa waandamizi huko Minova wiki iliyopita ambapo alitaka heshima ya ufanyaji kazi mzuri na kufuata haki za binadamu.

Radio Okapi inayomilikiwa na Umoja wa Mataifa ilisema jeshi liliwatambua watu waliohusika kwa ubakaji na wizi huko Minova na washukiwa hao walikamatwa.
 
Waasi wa kundi la M23 na makundi mengine yenye silaha pia yanakabiliwa na shutuma za unyanyasaji mbaya wa haki za binadamu uliofanyika katika wiki za karibuni. Serikali inalishutumu kundi la M23 kwa kuhusika na mauaji ya watu 64 katika muda wao mchache walioudhibiti mji wa Goma.
 
Umoja wa Mataifa unasema unachunguza ripoti 50 za ukiukaji mbaya wa haki za binadamu uliofanywa na kundi la M23 lilipoudhibiti mji huo.
mjadala huu umefungwa
Maoni
     
There are no comments in this forum. Be first and add one
 • Jioni
  30 min

  Jioni

  Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa...

 • VOA Express
  30 min

  VOA Express

  VOA Express ni matangazo mapya yenye mwendo wa kasi yakiangalia habari mpya za...

 • Alfajiri
  30 min

  Alfajiri

  Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za...

 • Jioni
  30 min

  Jioni

  Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa...

Mitaani

Your JavaScript is turned off or you have an old version of Adobe's Flash Player. Get the latest Flash player.
Matatizo ya Miundombinu Dar Es Salaami
|| 0:00:00
...  
🔇
X
21.05.2015 05:17
Wakazi wa Dar es Salaam wanasema ukosefu wa miundo mbinu inayostahiki ndiyo inasababisha matatizo ya uchafu, huduma za maji na nishati.