Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 05:16

Jee uhuru wa vyombo vya habari Tanzania uko hatarini


Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Tosamaganga, mkoani Iringa wakikimbia baada ya kufyetuliwa mabomu ya kutowa machozi na polisi
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Tosamaganga, mkoani Iringa wakikimbia baada ya kufyetuliwa mabomu ya kutowa machozi na polisi

Vyombo vya habari nchini Tanzania vimeendelea kukabiliwa na unyanyasaji kutoka askari wa jeshi la polisi wanapofuatilia ripoti za ghasia

Jeshi la polisi nchini Tanzania linalaumiwa kwa kufanya vitendo vya unyanyasaji dhidi ya waandishi wa habari hali iliyosababisha kuwakosesha haki wananchi kupata habari wanazostahili. Hiyo inatokana na vitendo vya hivi karibuni ambapo polisi wamekuwa wakiwakamata na kuwapiga waandishi habari wanapo ripoti juu ya maandamano au mikutano ya upinzan.

Jee uhuru wa vyombo vya habari Tanzania uko hatarini
Jee uhuru wa vyombo vya habari Tanzania uko hatarini


Tukiyo la karibuni lilitokea Jumatatu wiki hii wakati wanafunzi wa shule ya sekondari ya Tosamaganga mkoani iringa walipoandamana kwenda kwa mkuu wa mkoa wa Iringa kutoa malalamiko yao ya kukosa huduma bora shuleni. Polisi waliwashambulia wanafunzi na kuwatawanya kwa kuwafyetulia mabomu ya kutoa machaozi kwa madai kwamba hawakupata kibali cha kufanya maandamano hayo. Wakati huo huo baadhi ya waandishi habari walikamatwa na wengine kupigwa.

Baada ya kuhojiwa na Sauti ya Amerika kuhusiana na tukio hilo mwandishi habari Fransis Godwin alikamatwa siku ya Jumanne na kutiwa kizuizini mkoani Iringa, hali iliyochukiza waandishi wengine na kudai hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya unyanyswaji wa waandishi wa habari unaondelea nchini Tanzania.

Uhuru wa vyombo vya habari Tanzania

Abdusalim Kibanda mwenyekiti wa Jukwa la Wahariri nchini Tanzania anasema, jukwaa hilo limeanza utaratibu wa kupeleka malamiko kwa inspekta mkuu wa jeshi la polisi, Jenerali Saidi Mwema na baadae hatua nyingine zitafuata. Naye kamanda wa polisi mkoani Iringa Evaristi Mangara amekanusha unyanyaswaji wowote kufanywa kwa mwandishi huyo wa habari na kudai kuwa alikamatwa kuhojiwa.

XS
SM
MD
LG