Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 17, 2024 Local time: 01:39

Jaji Lubuva aahidi uchaguzi halali Tanzania


Mgombea uchaguzi wa upinzani -UKAWA , Edward Lowassa
Mgombea uchaguzi wa upinzani -UKAWA , Edward Lowassa

Mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi nchini Tanzania anasema tume yake inahakika uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika oktoba 25 utakuwa wa Amani na haki . mwandishi wa VOA Peter Clottey anatupasha zaidi katika taarifa inayosomwa na Harrison Kamau .

Jaji Damien Lubuva anasema kuwa tume ya uchaguzi ya kitaifa NEC inashirikiana kwa karibu na vyama vyote vya kisiasa kuelekea tarehe ya uchaguzi kuhakikisha kuna usawa wakati wa kupiga kura.

Baadhi ya wapinzani wameilaumu tume hiyo kwa kutokuwa na uwazi hasa baada ya kutoa orodha ya wapiga kura itakayotumika wakati wa uchaguzi.

Wanasema kama kutokuwa na uwazi kunaweza kushushia hadi yay a uhalali wa uchaguzi huo.

Lakini mwenyekiti wa tume hio jaji Lubuva hakubaliani nao, anasema kwa mara ya kwanza NEC itatumia mfumo wa kielektroniki kuwatambua na kutengeneza orodha ya wapiga kura kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika.

Lubuva anasema takriban wapiga kura milioni 24 wamesha jiandikisha. Anasema hili lilifanyika baada ya kukutana na washika dau wote na kuwaelezea kuhusu mfumo huo mpya.

Uchaguzi wa oktoba utakuwa wa nne tangu kuanzishwa mafumo wa vyama vingi vya kisiasa mwaka 1993. Uchaguzi wa mwaka huu unatarajiwa kuwa wenye ushindani mkubwa kufuatia kuhama kutoka chama tawala –CCM, aliekuwa waziri mkuu Edward Lowassa na kujiunga na chama cha upinzani, Chadema.

XS
SM
MD
LG