Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 04:43

Israel yatishia kuongeza mashambulizi yake Gaza


Waisrael wakitizama uharibifu wa jengo lililopigqwa na roketi iliyofyetuliwa kutoka Gaza
Waisrael wakitizama uharibifu wa jengo lililopigqwa na roketi iliyofyetuliwa kutoka Gaza
Mahambulizi ya kijeshi ya Israel katika ukanda wa Gaza inayotawaliwa na Hamas yameendelea kwa siku ya tano, huku wanaharakati wa Palestina hawajasita kufyetua roket kusini mwa Israel.

Katika mashambulizi hayo takriban Wapalestina 53 wameuwawa, miongoni mwao raia 24 na Waisrael 3 wameuliwa pia.

Israel imefanya mashambulio kadhaa ya ndege Jumapili huko Gaza, kwa kushambulia vituo vya kundi linalotawaka Hamas. Jeshi linasema ndege za kijeshi zimeshambulia vituo vya kufyetua roketi, kambi moja ya mafunzo na makao ya kijeshi. Vituo viwili vya habari vya wapalestina na waandishi wa kigeni vilishambuliwa pia katika mji wa Gaza.



Mashambulio yakiendelea juhudi za kidiplomasia zimekuwa zikifanyika kujaribu kusitisha mashambulizi kutoka pande zote mbili. Misri imeimarisha juhudi zake za upatanishi ikiwaalika wajumbe kutoka Hamas na Israel mijini Cairo.

Mwakilishi wa cheo cha juu wa Hamas Mousa Abu Marzook alikutana na maafisa wa Misri Jumapili na amesema Hamas inaunga mkono kurudi hali ya kawaida na kufikiwa makubaliano ya kusitisha vita. Misri inasema afisa muandamizi wa Israel amefika Cairo kwa mazungumzo ya kusitisha mapigano.
XS
SM
MD
LG