Jumanne, Aprili 28, 2015 Local time: 18:55

Habari / Afrika

ICC yasema Ngudjolo hana hatia

Mathieu Ngudjolo (kati) akisubiri kusomewa kesi yake huko ICC
Mathieu Ngudjolo (kati) akisubiri kusomewa kesi yake huko ICC
Mahakama ya kimataifa ya uhalifu-ICC imesema kiongozi wa wanamgambo wa Congo Mathieu Ngudjolo hana hatia ya uhalifu wa vita na uhalifu dhidi ya binadamu kuhusiana na shambulizi la mwaka 2003 lililosababisha vifo kwenye kijiji kimoja kiitwacho Bogoro mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC.

Waendesha mashtaka walimshutumu Ngudjolo kuwa aliwatumia watoto kama wanajeshi, aliongoza  mashambulizi dhidi ya raia na kwamba wapiganaji chini ya uongozi wake walifanya mauaji, ubakaji na vitendo vya wizi pamoja na utumwa wa ngono.

Mahakama ya ICC yenye makao yake The Hague ilisema Jumanne kwamba waendesha mashtaka walishindwa kuthibitisha uhusiano wa Ngudjolo na shutuma dhidi yake.

Shambulizi katika kijiji cha Bogoro kilichopo katika jimbo la Ituri nchini DRC lilisababisha vifo vya kiasi cha watu 20. Waathirika wengi walikufa kwa kukatwa mapanga.
 
Ngudjolo alipelekwa katika mahakama ya ICC mwaka 2009 pamoja na mshutumiwa mwingine, Germain Katanga ambaye bado anasubiri hukumu ya kesi yake. Wanasheria wa utetezi walisema watu hao wawili hawakuhusika na shambulizi hilo na walizishutumu serikali za Congo na Uganda kwa kupanga mauaji holela ili kuchukua tena udhibiti wa kijiji hicho kutoka kwa kundi la wanamgambo.

Mapigano kuhusiana na rasilimali za asili yalizuka huko Bogoro wakati vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Congo vikikaribia kumalizika.
mjadala huu umefungwa
Maoni
     
There are no comments in this forum. Be first and add one
 • VOA Express
  30 min

  VOA Express

  VOA Express ni matangazo mapya yenye mwendo wa kasi yakiangalia habari mpya za...

 • Alfajiri
  30 min

  Alfajiri

  Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za...

 • Jioni
  30 min

  Jioni

  Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa...

 • VOA Express
  30 min

  VOA Express

  VOA Express ni matangazo mapya yenye mwendo wa kasi yakiangalia habari mpya za...

Mitaani

Your JavaScript is turned off or you have an old version of Adobe's Flash Player. Get the latest Flash player.
Mbio za Boston Marathon, April 20, 2015i
|| 0:00:00
...  
🔇
X
21.04.2015 00:06
Mwanadada wa Kenya Caroline Rotich aliibuka mshindi wa mbio ndefu za Boston Marathon upande wa wanawake na Lelisa Desisa wa Ethiopia alirudia ushindi wake wa mwaka jana kwa kushinda mbio za wanaume siku ya Jumatatu April 20.