Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 00:33

ICC yakosa ushahidi dhidi ya Kenyatta


Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta atabasamu akiwa mahakamani huko The Hague, October 8, 2014.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta atabasamu akiwa mahakamani huko The Hague, October 8, 2014.

Wakili wa bwana Kenyatta,Steven Kay aliiambia mahakama ya The Hague Jumatano, kuwa inapaswa kufuta kesi dhidi ya mteja wake.

Mawakili wa rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wameiomba mahakama ya kimataifa -ICC, kufuta mashtaka ya uhalifu dhidi binadamu inayomkabili rais huyo.

Waendesha mashtaka katika mahakama hiyo ya ICC,wanasema hawana ushahidi wa kutosha kuendelea na kesi dhidi ya bwana Kenyatta ambaye anashtakiwa kwa kuhusika katika maandalizi ya ghasia za baada ya uchaguzi mkuu mwaka wa 2008 zilizosababisha mauaji ya zaidi ya watu 1,100.

Wakili wa bwana Kenyatta,Steven Kay aliiambia mahakama hiyo ya The Hague Jumatano, kuwa inapaswa kufuta kesi dhidi ya mteja wake.

Bwana Kenyatta ni rais wa kwanza anayehudumu kwenda mbele ya mahakama hiyo ya ICC. Jumatatu rais huyo wa Kenya alimwachia madaraka kwa muda naibu rais William Ruto ili aweze kuhudhuria kesi yake Jumatano.

Waendesha mashtaka wanasema serikali ya Kenya imewazuia kupata hati maalumu ikiwemo rekodi za mawasiliano ya simu ya bwana Kenyatta ili kuweza kuendelea na kesi hiyo.

Jumanne mwanasheria mkuu wa Kenya Githu Muigai, alisema serikali ya Kenya inafanya kila jitihada kutimiza madai ya mahakama hiyo lakini baadhi ya madai yake ni ngumu kutimilika.

XS
SM
MD
LG