Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 10:43

Hillary Clinton afanya ziara ya kushtukiza Libya


Waziri Clinton na rais wa Baraza la Kitaifa la Mpito Libya Bw.Mustafa Abdel Jalil mjini Tripoli Oktoba 18, 2011.
Waziri Clinton na rais wa Baraza la Kitaifa la Mpito Libya Bw.Mustafa Abdel Jalil mjini Tripoli Oktoba 18, 2011.

Waziri Clinton azungumza na utawala wa muda mjini Tripoli

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton amekwenda Libya Jumanne katika ziara ya kushtukiza na kukutana na viongozi wapya nchini humo huku wapiganaji wa serikali ya muda wakiendelea kupigana na wanajeshi watiifu kwa kiongozi wa zamani Moammar Ghadafi. Waziri Clinton aliwasili Tripoli leo Jumanne ambapo ameahidi msaada mpya wa mamilioni ya dola utakaotumiwa kwa program za elimu na afya kwa wapiganaji waliojeruhiwa katika vita nchini humo. Fedha hizo pia zitatumiwa kuharibu maelfu ya makombora ili kuyazuia kufikia wanamgambo. Maafisa wa Marekani wanasema msaada wake kwa Libya tangu mzozo kuibuka nchini humo umefikia dola milioni 135. Waziri Clinton alikutana na kaimu waziri mkuu Mahmud Jibril na mwenyekiti wa Baraza la Kitaifa la mpito Mustafa Abdel Jalil wakati wa zaiara yake. Ni afisa wa kwanza wa ngazi ya juu kutoka Marekani kwenda Tripoli tangu maasi kuanza dhidi ya Ghadafi mwezi Februari.

XS
SM
MD
LG