Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 13:26

Hali Bado Kizungumkuti Burundi


Picha ya Maktaba; rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, katikati, akisindikizwa katika uwanja a ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere International Airport, jinini Dar es Salaam, Tanzania, Mei 13, 2015.
Picha ya Maktaba; rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, katikati, akisindikizwa katika uwanja a ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere International Airport, jinini Dar es Salaam, Tanzania, Mei 13, 2015.

Hali nchini Burundi inazidi kuwa kitendawili huku kukiwa na taarifa zenye kutatanisha kutoka pande zinazopingana nchini humo.

Kundi linalompinga rais Pierre Nkurunziza linadai kushikilia maeneo muhimu nchini humo huku taarifa kutoka kwa serikali ikisema kuwa bado serikali iko thabiti chini ya uongozi wa Rais Nkrunziza.

Hata hivyo hali ya taharuki inaendelea kutanda kote nchini humo, huku raia wasijue cha kutarajia.

Kwa mujibu wa mwandishi wa Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika,mjini Bujumbura, Haidalla Hakizimana, milio ya risasi na milipuko imesikika usiku kucha na kufikia asubuhi ya Alhamisi.

Inasemekana kuwa radio binafsi zilikuwa zimeshambuliwa na wanaodaiwa kumuunga mkono rais Nkurunziza.

Raia walibaki majumbani kwa hofu ya kushambuliwa na kukosa uhakika wa nani mwenye mamlaka katika nchi kwa sasa.

Shughuli za kawaida kama usafiri zimekatizwa na wala hakuna watoto wanao hudhuria masomo hasa kwenye mji mkuu Bujumbura.

Wakati huohuo mwenyekiti wa chama cha madereva wa magari makubwa Tanzania, Clement Masanja amesema kuna magari kadhaa makubwa pamoja na madereva wamekwama nchini Burundi kufuatia matatizo haya ya kisiasa.

Anasema chama chake kimelazimika kusimamisha kwa muda usafirishaji mizigo kwenda nchini Burundi mpaka hali itakapokuwa nzuri.

Ameongezea kuwa chama chake kinafanya juhudi za kuwasiliana na mamlaka husika nchini Burundi kubuni njia za kuwarudisha nyumbani madereva wliokwama nchini humo.

XS
SM
MD
LG