Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 21:39

Haki za binadamu zapunguwa duniani


Nembo ya shirika la kutetea haki za binadamu
Nembo ya shirika la kutetea haki za binadamu

Mwaka wa 2012 ulishuhudia kuporomoka kwa demokrasia na haki za binadamu nchini Nigeria, Kenya na Somalia.

Wawakilishi wa kundi la kutetea haki za binadamu- Human Rights Watch, wanasema katika ripoti yao ya kila mwaka kwamba wana wasiwasi juu hali nchini Syria, Mali na nchi nyingine za kiarabu. Kundi hilo lenye makao yake New York lilitoa ripoti hiyo Alhamis katika miji ya London na Johannesburg.

Human Rights Watch linasema maandamano ya umma yaliyotokea katika nchi za kiarabu miaka miwili iliyopita hayakuimarisha haki kwa raia. Katika ripoti yake ya kurasa 665 iliyotolewa Alhamis kundi hilo linaelezea hali ya haki za binadamu katika nchi 80 ikiwemo Marekani, huku mzozo wa Syria ukiangazwa zaidi kwenye ripoti hiyo ambapo zaidi ya watu elfu 60 wamepoteza maisha yao.

Tiseke Kasambala mkurugenzi wa kundi hilo tawi la Afrika anasema hali barani humo nayo inazidi kuleta wasiwasi. “Mwaka wa 2012 ulishuhudia kuporomoka kwa maendeleo ya kidemokrasia na haki za binadamu pamoja na tishio la ugaidi katika nchi za Nigeria, Somalia na Kenya.”

Kasambala anasema mzozo unaoendelea Mali, Sudan na Sudan Kusini na vita katika Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo pamoja na Ethiopia na Eritrea, unahujumu maendeleo yaliyopatikana ya haki za binadamu na kanuni za kisheria katika bara la Afrika.
XS
SM
MD
LG