Ijumaa, Mei 29, 2015 Local time: 15:07

Habari / Afrika

Hagel akosa kuidhinishwa kama waziri wa ulinzi

Rais Obama akosoa maseneta wa chama cha Republican kwa siasa za mgawanyiko wakati Marekani ingali vitani Afghanistan.

Seneta wa zamani Chuck Hagel
Seneta wa zamani Chuck Hagel
       
 Maseneta  wa chama cha Republican wamezuia kura ya kumthibitisha mteuliwa wa rais Obama, Chuck Hagel kuwa waziri mpya wa ulinzi.

Baraza la Senate lilikosa  kura mbili tu Alhamisi  kuweza kumwidhinisha Hagel, kufuatia ombi la  Wademokrat kumaliza malumbano ya mdahalo wa muda mrefu na maseneta wa  chama cha Republican  juu ya uteuzi huo na kufikia  maamuzi ya mwisho.

Baraza la senate sasa linakwenda kwenye mapumziko ya siku 10  na itambidi bwana Bw. Hagel kusubiri muda huo wote  ili kuweza kujua ikiwa  atakuwa mkuu ajaye wa Pentagon.

Rais Obama alisema hatua ya maseneta wa chama cha Republican haikutarajiwa. Amesema pia inasikitisha kuona  maseneta wakitumia siasa za aina hiyo wakati Marekani ingali  vitani huko Afghanistan.

Wabunge wa chama cha Republican wanazuilia kuidhinishwa kwa Bw. Hagel, wakiitaka White House kutoa maelezo zaidi juu ya shambulizi la kigaidi la Septemba 11 mwaka jana katika ofisi za ubalozi wa Marekani mjini Benghazi, Libya.

Shambulizi hilo lilimwua balozi wa Marekani Christopher Stevens na Wamarekani wengine watatu. Lakini  Ikulu ya Marekani inasema imeshatoa maelezo ya kina kwa bunge juu ya shambulizi hilo.

Rais Obama alimchagua Hagel ambaye zamani alikuwa seneta wa chama cha Republican kuchukua nafasi ya waziri wa ulinzi anayeondoka Leon Panetta.
mjadala huu umefungwa
Maoni
     
There are no comments in this forum. Be first and add one
 • Alfajiri
  30 min

  Alfajiri

  Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za...

 • Jioni
  30 min

  Jioni

  Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa...

 • VOA Express
  30 min

  VOA Express

  VOA Express ni matangazo mapya yenye mwendo wa kasi yakiangalia habari mpya za...

 • Alfajiri
  30 min

  Alfajiri

  Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za...

Mitaani

Your JavaScript is turned off or you have an old version of Adobe's Flash Player. Get the latest Flash player.
Matatizo ya Miundombinu Dar Es Salaami
|| 0:00:00
...  
🔇
X
21.05.2015 05:17
Wakazi wa Dar es Salaam wanasema ukosefu wa miundo mbinu inayostahiki ndiyo inasababisha matatizo ya uchafu, huduma za maji na nishati.