Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 13:57

FAO yataka njaa na utapia mlo zitokomezwe


Kilimo cha mboga
Kilimo cha mboga

Maendeleo endelevu hayapatikani kukiwa na njaa

Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa- FAO, linasema maendeleo endelevu hayawezi kufikiwa hadi pale njaa na utapia mlo zitakapotokomezwa. Katika ripoti iliyotolewa Jumatano mkuu wa shirika hilo la FAO Jose Graziano da Silva, alisema lengo la maendeleo endelevu kamwe haliwezi kufikiwa ikiwa takriban mmoja kati ya watu saba duniani anakabiliwa na njaa au utapia mlo . Alitoa mwito wa kuongeza uzalishaji wa chakula na wakati huo huo kulinda mazingira ili dunia iweze kukidhi mahitaji ya chakula kwa watu wanaokisiwa kufikia bilioni tisa ifikapo mwaka wa 2050. FAO linasema kufanikisha lengo hilo lazima uwezekazji katika kilimo uongezwe kwa asili mia 60 katika miongo ijayo. Shirika hilo linaongeza kuwa robo tatu ya watu maskini duniani huishi vijijini ambapo wengi wanategemea kilimo kwa maisha yao. Ripoti ya shirika hilo la FAO imetolewa kabla ya mkutano ujao wa Umoja wa Mataifa unaotazamiwa kufanyika mjini Rio De Janeiro kuanzia Juni 20 hadi 22. Mchumi wa ngazi ya juu wa shirika hilo la chakula na kilimo duniani aliiambia sauti ya Amerika kuwa ajenda kuu ya mkutano huo itakuwa kutokomeza njaa duniani.

XS
SM
MD
LG