Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 12:57

Facebook yadaiwa kuhujuma usalama Kenya


Alama ya Facebook
Alama ya Facebook

Polisi wanaonya wananchi kutumia mitandao ya kijamii kwa tahadhari kubwa na kuepuka kueneza habari ambazo si za kweli au ambazo zinaweza kutumiwa kuhujumu usalama wananchi.

Usalama Kenya na mitandao
please wait

No media source currently available

0:00 0:02:34 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Utumiaji wa mitandao ya kijamii, hasa Facebook, nchini Kenya inatiliwa mashaka kwa madai ya kuhujumu usalama wa taifa, na sasa vyombo vya usalama nchini humo vinaonya wananchi dhidi ya kueneza uvumi.

Maafisa usalama wanasema kutokana na kuenea kwa matumizi ya mitandao ya kijamii habari za uvumi zinaenezwa kwa kasi na kuchukuliwa kama ukweli kwa sababu zipo katika mitandao.

Polisi wanaonya wananchi kutumia mitandao ya kijamii kwa tahadhari kubwa na kuepuka kueneza habari ambazo si za kweli au ambazo zinaweza kutumiwa kuhujumu usalama wananchi. Kamanda wa polisi katika County ya Kenya anasema ingawa wananchi wana haki ya kuwa na mitandao ya kijamii lakini wana wajibu pia wa kutumia mitandao hiyo kwa kuzingatia kanuni na masharti ya usalama nchini.

XS
SM
MD
LG