Jumapili, Mei 31, 2015 Local time: 01:24

Habari / Afrika

ElBaradei apinga uchaguzi wa bunge Misri

Wakristo wa Kanisa la Coptic wapinga tarehe ya uchaguzi wa bunge wakisema itaingiliana na sherehe za Pasaka.

Mohammed ElBaradei, kiongozi wa upizani Misri
Mohammed ElBaradei, kiongozi wa upizani Misri
Mmoja wa wapinzani wakuu wa kisiasa Misri ametoa mwito kwa raia kususia  uchaguzi ujao wa bunge. Mohammed ElBaradei amesema Jumamosi kuwa anakataa kushiriki katika uchaguzi ulioitishwa na rais Mohammed Morsi mapema wiki hii.

Bwana Morsi ameomba uchaguzi huo uanze Aprili 27, lakini maafisa wametangaza Jumamosi kuwa rais huyo anapanga kubadilisha tarehe hiyo kufuatia  upinzani kutoka  kwa waumini wa kanisa la Coptic, la Wakristo walio wachache. Tarehe ya Aprili 27 itaingiliana na sherehe za Kikristo za Pasaka.

Lakini Bw. ElBaradei ambaye zamani alikuwa mkuu wa idara ya nuklia ya Umoja wa Mataifa (I.A.E.A.)  alisema uchaguzi huo ni kisingizio tu na hutakuwa na matokeo ya hali halisi.

Chama cha Kiislam cha rais Morsi Muslim Brotherhood kimeshinda kila uchaguzi tangu kutimuliwa madarakani kwa rais wa zamani  Hosni Mubarak. Lakini mpaka sasa viongozi wengine wa upinzani hawajasema ikiwa wanaunga mkono wito  huo wa Bw. ElBaradei au watatii mwito wa rais huyo.
mjadala huu umefungwa
Maoni
     
There are no comments in this forum. Be first and add one
 • Je Nifanyeje?
  30 min

  Je Nifanyeje?

  Je Nifanyeje? Maamuzi ya Afya na Kijamii kwa Vijana - Kipindi cha dakika 30...

 • Jioni
  30 min

  Jioni

  Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa...

 • Jioni
  30 min

  Jioni

  Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa...

 • VOA Express
  30 min

  VOA Express

  VOA Express ni matangazo mapya yenye mwendo wa kasi yakiangalia habari mpya za...

Mitaani

Your JavaScript is turned off or you have an old version of Adobe's Flash Player. Get the latest Flash player.
Matatizo ya Miundombinu Dar Es Salaami
|| 0:00:00
...  
🔇
X
21.05.2015 05:17
Wakazi wa Dar es Salaam wanasema ukosefu wa miundo mbinu inayostahiki ndiyo inasababisha matatizo ya uchafu, huduma za maji na nishati.