Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 01:47

Kabila apendekeza majadiliano ya kisiasa DRC


Rais Joseph Kabila, wa Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo.
Rais Joseph Kabila, wa Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo.

Kabila alitaja kutokukubaliana juu ya orodha ya wapiga kura, ratiba ya uchaguzi, usalama wakati wa uchaguzi, yote ambayo anasema huwenda yakahujumu utaratibu mzima. Anasema chaguzi zilizopita za mwaka 2006 na 2011, zote ziligubikwa na ghasia baina ya vyama vya kisiasa.

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:00 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Rais wa Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, Joseph Kabila, anasema taifa lake litafanya kile alichokiita majadiliano ya kitaifa na kujumuisha mjadala wa kisiasa. Ajenda inaonekana kulenga juu ya uchaguzi, na baadhi ya wafuatiliaji wanaamini rais Kabila anatafakari juu ya mustakbal wake mwenyewe.

Hotuba ya rais Joseph Kabila imekuja wiki baada ya kuiomba umoja mataifa, kuja kusaidia kupeleka mwakilishi wa kimataifa, atakaye andaa majadiliano ya kisiasa. Katika hotuba yake iliyotangazwa jumamosi, Kabila alitaja sababu za kutiisha majadiliano hayo, ambayo yanahusiana na uchaguzi unaokuja.

Alitaja kutokukubaliana juu ya orodha ya wapiga kura, ratiba ya uchaguzi, usalama wakati wa uchaguzi, yote ambayo anasema huwenda yakahujumu utaratibu mzima. Anasema chaguzi zilizopita za mwaka 2006 na 2011, zote ziligubikwa na ghasia baina ya vyama vya kisiasa.

Kabila anasema, pia kuna maswali kuhusu jukumu la viongozi wa kisiasa walilonalo katika kuhamasisha uchaguzi wa amani.

Bw. Kabila aliuliza, kuna haja kweli ya watu kufanya ghasia nchini kwa sababu tu, walishindwa uchaguzi?

Kabila anasema, ufadhili pia litakuwa suala kuu, katika majadiliano hayo.

Anasema tume ya uchaguzi inakadiria mzunguko ujao wa uchaguzi utagharimu takriban dola billioni 1.2, huku serikali ikitegemea kuwa itagharimu dola millioni mia 5 pekee.

Kabila anasema kuanzia sasa, hatuwezi kufikiria kuhusu njia ya gharama nafuu ya kufanya uchaguzi, kama wanavyofanya katika nchi nyingine?

Mhariri wa gazeti la Congo news, Mike Mukebayi, anasema pendekezo hilo huenda likawa ni kidokezo kuwa Kabila na wafuasi wake wanataka kulielekeza taifa hilo katika uchaguzi usio wa moja kwa moja wa urais , kama ilivyofanyika katika nchi jirani ya Angola.

Mukebayi anasema, Pale Kabila anapozungumza, hazungumzi kama rais anayefikia mwisho wa awamu yake uongozi, anazungumza kana kwamba bado anataka kubakia madarakani.

Mukebayi anauliza, ni kwanini, iwapo rais ametambuwa kwamba kuna matatizo katika mfumo wa uchaguzi, anazungumzia masuala hayo wakati huu, pale anapomalizia awamu yake, pale ambapo hilo sio tena tatizo lake?

awamu ya pili madarakani ya Kabila, inatarajiwa kufikia hatima yake mwisho wa mwezi December mwaka 2016.

Chama kikuu cha upinzani nchini Congo, UDPS kimesema, kiko tayari kwa majadiliano na mpatanishi wa kimataifa.

Lakini baadhi ya vyama vingine vya upinzani vinapinga wazo hilo la majadiliano, vikisema Kabila huwenda akatumia kubakia madarakani.



XS
SM
MD
LG