Alhamisi, Novemba 26, 2015 Local time: 01:18

Habari

Donna Summer afariki kutokana na saratani

Mwimbaji huyo mashuhuru aliyejulikana kama Malkia wa Disco aliwafurahisha watu wa vizazi mbali mbali.

Mwimbaji Donna Summer
Mwimbaji Donna Summer

Donna Summer aliyeimba moja wapo ya nyimbo mashuhuri "Hot Stuff", aliweza kuwafurahisha watu miaka mingi baada ya kuacha mtindo huo wa Disco ulokua mashuhuri katika miaka  1970 na 1980.

Licha ya umashuhuri huo wote alionekana hakuwa na rahakuwa mashuhuri kwani alisema, wakati wowote mafanikio yanapopatikana basi inakua jambo geni."

Alizaliwa akiwa na jina la Donna Gaines hapo Disemba 31, 1948 mjini Boston, Massachusetts, na katika maisha yake aliweza kujinyakulia mara tano tunzo mashuhuri na kuu la muziki la Marekani Grammy.

kama waimbaji wengi mashuhuri wa Marekani wa makamu yake alinaza kuimba katika kwaya ya kanisa. Alipofika shule ya sekondari alianza tayari kucheza katika micehzo ya kuiga ya shule na wiki chache kabla ya nkuhetimu alikua katika mchezo wa kuigiza wa uwimbaji "Hair", jukumu lililompeleka hadi Ujerumani.

Huko Ujerumani alibaki kwa muda na mwajka 1974 akarikodi santuri yake ya kwanza, "Lady of the Night."

baada ya muziki wa Disco kutoweka Summer aliendelea kuimba na kuwatumubwiza mashabiki wake, hadi kufariki mapema Alhamisi katika jimbo la Florida ambako alikua anaishi na mumewe muimbaji Bruce Sudano

You May Like

video Maoni ya Papa Francis yanayotofautiana na Waafrika

Muelekeo wa Papa Francis wa kufanya mabadiliko muhuimu katika Kanisa lam Katholiki yanatofautiana kwa kiwango fulani na maoni ya waumini wa kiafrika. Zaidi

sauti Zanzibar: Vikao vingi bila suluhisho

Vikao vinne tayari vimefanyika katika Ikulu ya Zanzibar na kuwashirikisha viongozi mbalimbali wakiwemo wa zamani na wa sasa tangu kuzuka kwa mzozo wa matokeo ya uchaguzi lakini hakuna tamko rasmi mpaka sasa. Zaidi

Multimedia Pope Francis Begins African Tour

His schedule in Nairobi includes meetings with President Uhuru Kenyatta and a group of diplomats at the State House Zaidi

mjadala huu umefungwa
Maoni
     
There are no comments in this forum. Be first and add one