Jumanne, Mei 26, 2015 Local time: 08:27

Habari / Marekani

Clinton ajibu wakosoaji vikali.

Waziri Clinton akijibu maswali ya wabunge kuhusu Libya.
Waziri Clinton akijibu maswali ya wabunge kuhusu Libya.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton amejitetea vikali  kutokana na  lawama  za jinsi alivyosimamia wizara hiyo wakati wa  mashambulizi mabaya ya Septemba 11 katika ubalozi mdogo wa Marekani huko Benghazi ,Libya na kupinga ukosoaji wa baadhi ya wabunge kwamba kulikuwa na jaribio la kuwahadaa wananchi wa Marekani juu ya kile kilichotokea .

Akijitetea vikali  waziri Clinton alitoa ushahidi  Jumatano mbele ya kamati mbili za bunge zinazochunguza shambulizi hilo ambalo lilimuuwa balozi wa Marekani Christopher Stevens na wamarekani wengine watatu .
Mahojiano na Mitinyi
Draft Entryi
|| 0:00:00
...    
🔇
X

Clinton aliiambia kamati ya mambo ya nje ya bunge anawajibika kwa mapungufu yaliotokea  katika ulinzi kwenye ubalozi mdogo wa Marekani huko Benghazi .

 Akitoa majibu  katika kikao hicho  waziri  Clinton alisema kutokuwa na uthabiti huko Mali kunapelekea kuwepo kwa eneo salama la magaidi ambao wanatafuta  hifadhi  katika maeneo ya kaskazini mwa Afrika.

Aliongeza kuwa  Marekani na washirika wake wamekuwa wakifanya kazi na majirani wa Mali ili kuongeza usalama lakini wengi hawana uwezo wa kufanya hivyo.

Maelezo yake yametolewa  wakati ongezeko la majeshi ya Ufaransa na Afrika yakiingia Mali kusaidia jeshi la nchi hiyo kuwaondoa wanamgambo wa kiislam kutoka kwenye ngome yao huko kaskazini.
mjadala huu umefungwa
Maoni
     
There are no comments in this forum. Be first and add one
 • Alfajiri
  30 min

  Alfajiri

  Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za...

 • Jioni
  30 min

  Jioni

  Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa...

 • VOA Express
  30 min

  VOA Express

  VOA Express ni matangazo mapya yenye mwendo wa kasi yakiangalia habari mpya za...

 • Alfajiri
  30 min

  Alfajiri

  Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za...

Mitaani

Your JavaScript is turned off or you have an old version of Adobe's Flash Player. Get the latest Flash player.
Matatizo ya Miundombinu Dar Es Salaami
|| 0:00:00
...  
🔇
X
21.05.2015 05:17
Wakazi wa Dar es Salaam wanasema ukosefu wa miundo mbinu inayostahiki ndiyo inasababisha matatizo ya uchafu, huduma za maji na nishati.