Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 08:45

Clinton aongoza kwa wagombea urais wa Democrat


Wagombea urais wa Democrat (L) Martin O'Malley, Hillary Clinton na Bernie Sanders katika mdahalo huko Gaillard Center mjini Charleston, S.C., Jan. 17, 2016.
Wagombea urais wa Democrat (L) Martin O'Malley, Hillary Clinton na Bernie Sanders katika mdahalo huko Gaillard Center mjini Charleston, S.C., Jan. 17, 2016.

Wagombea watatu wa urais kutoka chama cha Democrats walifanya mdahalo wao wa mwisho Jumpili usiku mbele ya wapigakura na kuongeza uwezo wao kwenye uchaguzi wa awali katika jimbo la Iowa.

Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani, Hillary Clinton, seneta wa Vermont, Bernie Sanders na gavana wa zamani wa jimbo la Maryland, Martin O’Malley walikutana kwa mara ya nne kujadili masuala kadhaa ambapo mdahalo wa Jumapili ulifanyika katika mji wa Charleston kwenye jimbo la South Carolina.

Sanders (L), Hillary na O' Malley katika mdahalo wa Dec. 19, 2015.
Sanders (L), Hillary na O' Malley katika mdahalo wa Dec. 19, 2015.

Uchunguzi mpya wa maoni wa kituo cha televisheni cha NBC News na Wall Street walitoa takwimu zao kabla ya mdahalo kuanza na kuonesha Clinton akiongoza mbele ya Sanders kwa asilimia 25 kiwango cha kitaifa.

Uchunguzi wa kwanza wa maoni wa Clinton ulikua asilimia 59 za wapigaji kura wadogo wa Democrat wakati Sanders alipata asilimia 34 ya wanaomuunga mkono. O’Malley alipata kiasi cha asilimia 2 na mdahalo huo wa Jumapili utaweza kuwa fursa yake ya mwisho ya kuwashawishi wapigakura kwamba anastahili kuteuliwa kuwa mgombea urais wa chama cha Democrat.

XS
SM
MD
LG