Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 09:54

China yapeleka jeshi la kulinda amani Sudan Kusini


Walinda amani wa jeshi la Umoja wa Mataifa wakiwa katika mji mkuu Juba nchini Sudan Kusini
Walinda amani wa jeshi la Umoja wa Mataifa wakiwa katika mji mkuu Juba nchini Sudan Kusini

China inapeleka mamia ya wanajeshi kuungana na jeshi la kulinda amani la Umoja wa Mataifa katika eneo lenye vita nchini Sudan Kusini mahala ambako makampuni ya China yana maslahi makubwa ya mafuta.

Matamshi kutoka kwa Wizara wa Mambo ya Nje wa China Jumanne yalifuatia ripoti katika gazeti la Wall Street Journal la Marekani kwamba China inapeleka wanajeshi kulinda viwanda vya mafuta nchini Sudan Kusini na kuwapatia ulinzi wafanyakazi wa China.

Akijibu maswali ya waandishi wa habari, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Hua Chunyinf hakutoa maelezo yeyote juu ya mafuta au makampuni ya China, akisema lengo la China ni kufuata kwa makini mwongozo wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kuhamasisha ujenzi katika eneo hilo.

Hua alisema China tayari imeshapeleka walinda amani 1,800 nchini Sudan Kusini huku msemaji wa operesheni za Umoja wa Mataifa nchini humo Joe Contreras akisema Beijing ilipanga kupeleka wanajeshi 700, lakini hakuna hata mwanajeshi mmoja aliyewasili.

Hakukuwa na maelezo ya haraka juu ya mkanganyiko wa idadi kamili ya wanajeshi wanaokwenda nchini Sudan Kusini.

Gazeti la Wall Street Journal linasema kampuni ya taifa ya mafuta China inamiliki hisa ya asilimia 40 katika hisa za pamoja ambazo zinaendesha viwanda vya mafuta vya Sudan Kusini na pia inaendesha bomba la usafirishaji nje mafuta lenye kilomita 1,000 ambalo linasafirisha mafuta ghafi kupitia nchi jirani ya Sudan.

Uzalishaji mafuta umeingia kasoro kwa miezi kadhaa ya ghasia zilizozuka kutokana na mzozo wa kisiasa kati ya Rais Salva Kiir na naibu wake wa zamani Riek Machar.

XS
SM
MD
LG