Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 19:30

Marekani yasimamisha misaada ya kiusalama Burundi


Watu wakiwa msitarini kupiga kura ya bunge June 29 nchini Burundi
Watu wakiwa msitarini kupiga kura ya bunge June 29 nchini Burundi

Marekani inasema inasitisha baadhi ya misaada yake ya usalama kwa Burundi kutokana na unyanyasaji unaofanywa na polisi wakati wa maandamano ya kisiasa na uamuzi wa serikali kuendelea na kile Marekani ilichokiita uchaguzi wa bunge uliokuwa na kasoro.

Wizara ya Mambo ya Nje ilisema Alhamisi usiku kwamba uamuzi wa Rais wa Burundi Pierre Nkurunzinza kugombea muhula wa tatu kumepelekea vifo vya darzeni ya watu, wimbi la zaidi ya warundi 144,000 kukimbilia katika nchi za jirani na kuanguka kwa uchumi wa Burundi.

Taarifa hiyo inaeleza kwamba uamuzi wa serikali kuendelea na uchaguzi wa bunge wa Juni 29 licha ya kutokuwa na hali ya huru na haki imepelekea kusababisha hali iliyokuwa tayari tete kuwa mbaya zaidi. Marekani imeitaka Burundi kusikiliza wito wa jumuiya ya kimataifa kusogeza mbele uchaguzi wa rais wa Julai 15.

Mapema Alhamisi Umoja wa Mataifa ulisema kuwa uchaguzi wa bunge Jumatatu nchini Burundi haukuwa huru na wa haki. Vyama vya upinzani vilisusia uchaguzi huo.

XS
SM
MD
LG