Jumatano, Mei 22, 2013 Local time: 11:54

Habari / Afrika

Bunge jipya Somalia laanza kazi

Serikali kuu ya muda iliundwa mwaka 2004 na haijaweza kuwa na nguvu ya kutosha kuleta uthabiti nchini humo

Rais wa Somalia Sheikh Sharif Sheikh Ahmed(C) akipeana mkono na mwakilishi maalumu wa UN kwa Somalia, Augustine Mahiga(R)
Rais wa Somalia Sheikh Sharif Sheikh Ahmed(C) akipeana mkono na mwakilishi maalumu wa UN kwa Somalia, Augustine Mahiga(R)
ukubwa wa habari - +
Bunge jipya la  Somalia limeanza kazi  jumatatu wakati nchi hiyo inasonga mbele na mpango wa kuunda  serikali thabiti ya kudumu.

Kamati ya uchaguzi imewataja wabunge 225 kati ya viti 275 vilivyopo lakini maafisa wanasema idadi hiyo inatosha kwa bunge kufanya kikao chake.

Katika mahojiano na Sauti ya Amerika-VOA waziri wa katiba na maridhiano, Abirahman Hosh Jibril anasema wabunge wapya watamchagua spika na manaibu ifikapo Agosti 27 na Rais mpya wa Somalia ifikapo mwanzoni mwa mwezi Septemba.

Nchi hiyo imevuka tarehe ya mwisho ambayo ni jumatatu ya kumchagua spika mpya na Rais chini ya mpango uliopendekezwa na Umoja wa Mataifa ili kumaliza mamlaka ya serikali ya muda iliyohudumu kwa miaka minane.

Hata hivyo, maafisa wa Umoja wa Mataifa na washirika  wa kimataifa walitoa taarifa ya matumaini jumapili wakisema Somalia ina fursa  ya kipekee ya kuleta amani na uthabiti.

Mwezi uliopita wajumbe 825 wa bunge  walipitisha katiba mpya.

Somalia imekuwa katika miaka 20 ya vurugu na mgogoro tangu wababe wa kivita walipompindua Rais Mohamed Siad bare mwaka 1991.

Serikali kuu ya muda iliundwa mwaka 2004 na haijaweza kuwa nguvu ya kutosha na kuleta uthabiti katika nchi iliyoharibiwa na  vurugu  kwasababu ya mapigano sugu ya ndani.

Usalama umeimarika katika mji mkuu, Mogadishu tangu jeshi la Umoja wa Afrika lilipolisukuma nje kundi la  wanamgambo la al-Shabab mwaka jana. Lakini kundi  hilo bado linafanya mashambulizi ya mara kwa mara mjini humo.
mjadala huu umefungwa
Maoni
     
There are no comments in this forum. Be first and add one

Mitaani

Loading
12:00:00 / -:--:--