Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 13:26

Balozi mpya wa Marekani aahidi kuimarisha ushirikiano na Uganda

Balozi Deborah Malac (katikati) wakati wa usafiri wake nchini Liberia. Kamati ya masuala ya kigeni ya baraza la Seneti la Bunge la Marekani, Jumanne lilisikiliza ushahidi wa Balozi huyo aliyeteuliwa kuwakilisha Marekani Nchini Uganda.

Kamati ya masuala ya kigeni ya Baraza la Senet la Bunge la Marekani, lilianza utaratibu wa kusikiliza ushahidi wa mabolozi wa Marekani waloteuliwa kupelekwa Uganda Malawi na Swaziland.

Kamati ya masuala ya kigeni ya Baraza la Senet la Bunge la Marekani, lilianza utaratibu wa kusikiliza ushahidi wa mabolozi wa Marekani waloteuliwa kupelekwa Uganda Malawi na Swaziland.

Katika Kikao hicho cha Jumanne asubuhi, Seneta Chris Coons alimuliza Balozi Deborah R Malac, anaeteuliwa kupelekwa Uganda jinsi atakavyoweza kuwanisha jukumu lake la kuhamasisha demokrasia na uhuru wa mashirika ya kiraia na kuweka sawa ushirikiano na mshirika wa karibu wa usalama.

Bi. Malac amesema, utaratibu wa kuleta demokrasia unayofanya kazi kama inavyohitajika ni utaratibu unaochukua muda. Kwa hivyo, anasema ukikumbuka na kulinganisha uchaguzi ulofanyika miaka kadhaa iliyopita, na uchaguzi utakaofanyika mwakani kuna tofauti kubwa inayoanza kufanana na utaratibu huo wa demokrasia. Hata hivyo amesisitiza ingali iko katika hali ya mparaganyiko, na haijaota mizizi huko Uganda kama wengi wetu tungelivyopenda kuona.

Kwa hivyo Bi Malac anasema akiidhinishwa kuwa balozi ataendelea mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea na Rais Museveni kumueleza kwamba mabadiliko ni jambo zuri, “mara nyingine mawazo mepya tofauti huleta nafasi nyingine nzuri. Lakini muhimu Zaidi nikumhimiza kuruhusu vyama vya upinzani, mashirika ya kiraia na waganda, kuwa na sauti ya kupendekeza maendeleo ya nchi yao. Kuwawezesha wanasiasa wa upinzani na kubuni upinzanoi wa kweli kwa nchi hiyo.

Utaratibu wa kuidhinisha mabalozi hao unatazamiwa kumalizika mwishoni mwa wiki.

XS
SM
MD
LG