Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 09:28

Mwai Gikonyo, mwandishi wa VOA aaga dunia


Mwai Gikonyo (kushoto) akizungumza na Festus Mogae rais wa zamani wa Botswana
Mwai Gikonyo (kushoto) akizungumza na Festus Mogae rais wa zamani wa Botswana

Kwa masikitiko makubwa Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika inatangaza kifo cha mwandishi wake wa muda mrefu wa Nairobi, Mwai Gikonyo, aliyefariki Jumatatu Februari 8, 2016 baada ya kuugua saratani ya utumbo.

Gikonyo amekuwa mwandishi habari wa VOA tangu mwanzoni mwa miaka 1990, akiripoti matukio yote muhimu ya Kenya, na Afrika Mashariki, akiwa mwandishi aliyebobea na mahiri wa vyombo vya habari vya kimataifa.

Daima alipendelea kuwa miongoni mwa waandishi wa habari wa kwanza kupata habari muhimu na kuripoti kabla ya mtu mwingine yeyote. Alifahamu vyema siasa za Kenya na kuwa na uhusiano mzuri na waandishi wenzake.

Gikonyo, aliyezaliwa Oktoba 6 1952, alitumikia vyombo mbali mbali vya habari huko Kenya ikiwa ni pamoja na Shirika la utangazaji nchini humo, KBC, kabla ya kujiunga na vituo vya matangazo vya kimataifa. Miongoni mwa stesheni za kimataifa alizowahi kufanyia kazi ya utangazaji ni Sauti ya Ujerumani, radio ya Uholanzi, na redio ya taifa ya Afrika Kusini, SABC.

Bw Gikonyo amemuacha mke na watoto wawili. Sauti ifuatayo ambayo wengi walikuwa wameizoea, na ambayo mashabiki, watangazaji na wafanya kazi wote wa idahaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika wataikumbuka daima, imetoweka.

Ripoti ya Mwai Gikonyo juu ya mgomo wa walimu
please wait

No media source currently available

0:00 0:03:18 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

XS
SM
MD
LG