Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 05:08

Australia yapata waziri mkuu mpya


Waziri Mkuu wa Australia Tony Abbott
Waziri Mkuu wa Australia Tony Abbott

Waziri mkuu wa Australia Tony Abbott, ameondolewa kwa ghafla madarakani Jumatatu, Septemba 14 2015, kutokana na kura ndani ya chama chake cha Liberal Party, kufuatia kupunguka kwa umashuhuri wake katika uchunguzi wa maoni ya wananchi.

Nafasi yake inachukuliwa na mkuu wa chama hicho cha mrengo wa kushoto Bw. Malcom Turnbull aliyekua waziri wa mawasiliano katika serikali ya mungano.

Turnbull alijipatia kura 54 dhidi ya 44 ya Bw Abbott, huku wabunge wa chama hicho cha Liberal kupiga kura kumacha Bi. Julie Bishop katika nyadhifa yake ya naibu wa chama.

please wait

No media source currently available

0:00 0:07:11 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Mabadiliko hayo yanafikisha kikomo msukosuko mkubwa wa kisiasa Australia ambapo wanachama wa chama cha kisiasa wanaweza kumshambulia kiongozi wao kwa kushtukiza na kumondowa madaraka.

Gode Migerano
Gode Migerano

Mhariri wa Idhaa ya Kiswahili ya redio SBS huko Sydney, Australia, Gode Migerano, anasema yaliyofanyika ndani ya chama cha Liberal ni mapinduzi ya uwongozi na hivi sasa ni kusubiri na kuona ikiwa waziri mkuu mteule Turnbull ataitisha uchaguzi wa mapema au atabaki na kumaliza muhula wa aliyemtangulia hapo mwakani.

XS
SM
MD
LG