Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 14:04

Rais wa Marekani, Barack Obama amewasili nchini Kenya.


Rais wa Marekani, Barack Obama akiwasili nchini Kenya akiwa na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta .Julai 24,2015.
Rais wa Marekani, Barack Obama akiwasili nchini Kenya akiwa na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta .Julai 24,2015.

Rais wa Marekani, Barack Obama amewasili nchini Kenya, huku kukiwa na ulinzi mkali sana, ikiwa ni mwanzo wa ziara ya siku mbili nchini humo.

Rais Obama alilakiwa na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya. Rais wa Marekani aliepeana mikoni na viongozi wengine wa Kenya na kutia sain kitabu maalum cha wageni kabla ya kupanda kwenye gari yake.

Mitaa ya Nairobi ilikuwa imepakawa rangi na kusafishwa, mji ulitumia kila ilichokuwa nacho kwa ajili ya kumkaribisha Obama kwa kile ambacho wakenya wamekiita “kurejea nyumbani.”

Mkutano wa kimataifa wa wajasiriamali wa Global Entreprenuership Summit kwa mara ya kwanza unafanyika barani Afrika. Rais Obama akiwa mmoja wa wenyeji wa mkutano huo atahutubia katika mkusanyiko wa GES siku ya Jumamosi.

Kenya pia ina umuhimu maalum kwa rais wa Marekani. Baba yake Obama alizaliwa na kuzikwa katika eneo la vijijini magharibi mwa kenya na kutumika katika serikali wakati wa utawala wa rais wa kwanza wa Kenya.

Obama aliitembelea Kenya mwaka 2006 alipokuwa Seneta wa Marekani, lakini, hii ni ziara yake ya kwanza kama rais. Naibu rais wa Kenya, William Rutto amesema ziara hii ina maana kubwa kwa nchi yake.

“Rais Obama siyo tu kama rais mwingine yoyote wa Marekani. Ana mizizi ya kiafrika, na ana asili ya Kenya na huu ni umuhimu kwa njia tofauti kabisa, amesema Rutto.

XS
SM
MD
LG