Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 17:47

Mamillioni ya watoto Yemen watishiwa na magonjwa


Watoto nchini, Yemen.
Watoto nchini, Yemen.

Idara ya Umoja Mataifa ya kuhudumia watoto UNICEF, inaonya kwamba mamillioni ya watoto katika taifa linalokumbwa na vita la Yemen wanatishiwa na utapia mlo na wako katika hatari ya kukumbwa na magonjwa mabaya yanayoweza kuzuilika kama vile surua ya homa ya mapafu.

Vita nchini Yemen vinasababisha athari mbaya kwa watoto nchini humo. Ripoti ya UNICEF inaeleza kuwa, takriban watoto 279 wameuwawa na wengine 402 kujeruhiwa tangu mwishoni mwa mwezi marchi, pale Saudia Arabia ilipoanza kampeni yake ya mashambulizi ya anga dhdi ya waasi wa Kihouthi.

UNICEF inaripoti kuwa watoto takriban 318 wameandikishwa kama wanajeshi, lakini inasema inaamnini idadi ya kweli ya waioandikishwa ni kubwa Zaidi.

Wakati takwimu hizo zinashutusha, UNICEF inasema watoto pia wanakabiliwa na hatari za magonjwa na utapia mlo. Msemaji wa UNICEF Christof Boulierac, anasema watoto wako hatarini kupata magonjwa yanayoweza kuzuilika kwa sababu hawajapatiwa chanjo.

Kwasababu ya mzozo, Boulierac anasema vituo vya afya havina umeme wala mafuta wanayohitaji kuhifadhi chanjo kwenye mahala baridi. Anasema watoto wengi pia wanakosa chanjo za kuokowa maisha kwa sababu wazazi wao mara nyingi wanakhofia mapigano kuwapeleka kupata chanjo.

UNICEF inasema idadi ya watoto waliokumbwa na maambukizo ya mabaya ya magonjwa hatari ya kupumua imeongezeka maradufu hadi watoto millioni 1.3 tangu marchi. Hii inaashiria ongezeko kubwa lakutokuwa na uwezo kwa watoto kupata matibabu yanayohitajika kwasababu mahospitali na kliniki hazifanyi kazi sawa sawa.

Ripoti inasema maji machafu , hali duni za usafi wa vyoo na ukosefu wa madini ya chumvi mwilini kunawaweka watoto zaidi ya millioni 2.5 katika hatari ya kupata magonjwa ya kuharisha, ambayo mara nyingi ni hatari. Boulierac anasema utapia mlo pia ni tishio linaloongezeka.

Boulierac anasema UNICEF na washirika wake wanafanya kila wawezalo kuwapatia chanjo watoto na kuwapatia lishe ya kuokowa maisha kwa watoto wenye walioathirika na utapia mlo, lakini anasema kuwapatia huduma zinazohitajika ni changamoto kubwa sana.

XS
SM
MD
LG