Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 11:01

Rais wa Burundi ajitokeza hadharani


Rais Pierre Nkurunziza akizungumza katika makazi ya Rais Bujumbura, Burundi, Mei 17, 2015.
Rais Pierre Nkurunziza akizungumza katika makazi ya Rais Bujumbura, Burundi, Mei 17, 2015.

Rais wa Burundi Pierre Nkurunzinza ameonekana mbele ya umma kwa mara ya kwanza Jumapili tangu jaribio la mapinduzi lililoshindwa wiki iliyopita.

Aliwasalimu waandishi wa habari jumapili katika makazi yake kwenye mji mkuu Bujumbura.

Katika hotuba kwenye radio Ijumaa, Nkurunzinza alishukuru vikosi vya usalama kuzuiya jaribio la mapinduzi ya kijeshi dhidi ya serikali yake.

Pia alionya waandamanaji kuacha maandamano yao dhidi ya uamuzi wake wa kutaka kugombea muhula wa tatu.

Wanaharakati, hatahivyo wameitisha maandamano zaidi kumpinga rais huyo na uamuzi wake wa kutaka kuingia tena madarakani ambao wanasema ni kinyume cha katiba.

Rais na wafuasi wake wamedai kwamba kipindi cha tatu kinaruhusiwa kwa sababu alichaguliwa na bunge , na siyo wapiga kura katika kipindi chake cha kwanza cha mwaka 2005.

Mahakama ya katiba nchini Burundi imekubaliana na rais. Marekani iliwahi kusema kuwa bwana Nkurunzinza asigombee tena urais.

waziri msaidizi wa mambo ya ndani wa Marekani Linda Thomas –Greenfield ameiambia sauti ya Amerika kwamba uamuzi huo unasababisha ukosefu wa uthabiti ndani ya nchi.

XS
SM
MD
LG