Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 11:15

Marekani na Umoja wa Mataifa zapeleka wajumbe maalum Burundi


Wafuasi wa upinzani wakiandamana katika mji mkuu wa Bujumbura Burundi.
Wafuasi wa upinzani wakiandamana katika mji mkuu wa Bujumbura Burundi.

Marekani, Umoja wa Matiafa, Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika zina mhimiza rais Pierre Nkurunziza wa Burundi kuheshimu katiba wakati ghasia na maandamano yakiendelea nchini humo tangu uwamuzi wake wa Jumamosi April 25 kutangaza anagombania tena mhula mwengine.

Tom Malinowski
Tom Malinowski

Rais Barack Obama amemtuma naibu waziri wa mambo ya nchi za nje kwa ajili ya demokrasia, haki za binadam na kazi Tom Malinowiski, hadi Bujumbura akiwa na ujumbe wa kuwahimiza wakuu wa nchi hiyo kutochukua hatua ambazo zitaweza kutumbukiza nchi hiyo katika hali isiyoweza kurekebishwa tena.

"Ujumbe wangu kwa wakuu wa Burundi ni kwamba muda haujapita bado kuonesha uwongozi, muda haujapita kuonesha ustahmilivu na kuepusha kutumia ghasia. Na muda haujapita kuwazuia baadhi ya vijana wenye silaha na wengine walohusika katika ghasia siku za nyuma. Msichukuwe hatua ambazo mtakuja kujuta."

Bw Malinowski anasema bado kuna muda na nafasi ya majadiliano, kwani anasema Burundi imeweza kufanya maendeleo makubwa katika kurudisha hali ya utulivu baada ya vita vibaya vya wenyewe kwa wenyewe karibu miaka 10 iliyopita.

Umoja wa Mataifa wapeleka ujumbe.

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban ki Moon anatuma mwakilishi wake maalum kwa Kanda ya Maziwa Makuu huko Burundi Said Djinnit, kwa mashauriano na maafisa wa serikali, Rais Nkurunzinza na viongozi wa vyama vya siasa.

Katibu Mkuu Ban, amewataka wakuu wa idara za usalama wa Burundi kufanya kazi kwa weledi na kwa pande zote kuachana na ghasia na kuepuka hotuba zenye kuchochea chuki.

Mwenye kiti wa tume ya Afrika, Nkosazana Dlamini Zuma ametowa wito Jumapili kupitia ujumbe wa Twitter, kuwataka viongozi wa Burundi kujaribu kuonesha ustahmilivu kwa waandamanaji wanaopiga mhula wa tatu wa rais

please wait

No media source currently available

0:00 0:14:00 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Katibu mkuu wa zamani wa chama tawala cha CNDD-FDD, Hussein Rajabu akiwa uhamishoni anasema ni jambo la kusikitisha yanayotokea lakini ana uhakika warundi watapata ushindi katika kulinda mafanikio walopata tangu makubaliano ya Arusha.

Kundi la wakimbizi wa Burundi wakisubiri msaada huko Bugesera, Rwanda.
Kundi la wakimbizi wa Burundi wakisubiri msaada huko Bugesera, Rwanda.

Watu wasiopungua sita wamefariki dunia wiki hii katika mapambano kati ya Polisi na waandamanaji katika mji mkuu Bujumbura, na maelfu ya warundi wameshakimbia hadi nchi jirani za Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakihofia ghasia zinaweza kuzuka tena nchini mwao.

XS
SM
MD
LG