Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 08:55

Rubani msaidizi wa Germanwings aliangusha ndege kwa makusudi


Ndege ya Germanwings Airbus A320 iliyosajiliwa kwa D-AIPX ilivyoonekana kwenye uwanja wa ndege wa Berlin, March 29, 2014
Ndege ya Germanwings Airbus A320 iliyosajiliwa kwa D-AIPX ilivyoonekana kwenye uwanja wa ndege wa Berlin, March 29, 2014

Mwendesha mashtaka mmoja wa Ufaransa anasema rubani msaidizi wa ndege ya kampuni ya Germanwings ambayo ilipata ajali katika milima ya French Alps wiki hii alifanya “jaribio la makusudi la kuiangusha ndege”.

Mwendesha mashtaka wa Marseilles, Brice Robin alisema Alhamis kwamba rubani mwenza, Andreas Lubitz mwenye umri wa miaka 28 alimfungia rubani nje ya chumba cha marubani na kubaki mwenyewe akidhibiti ndege aina ya Airbus A320.

Mwendesha mashtaka alisema Lubitz kisha “aliongeza mwendo na kuishusha ndege kwa makusudi” ikiruka kwa kasi ya kilomita 700 kwa saa na kusababisha ajali katika eneo moja dogo kwenye milima yenye theluji huko kusini-mashariki mwa Ufaransa na kuuwa watu wote 150 waliokuwemo ndani.

“Ajali hiyo inaweza kutokea tu kwa kufanyika tendo la makusudi”, Robin alisema katika mkutano na waandishi wa habari. “Kwa namna yeyote ile, ni tukio la kukusudia”

Chansela wa Ujerumani, Angela Merkel
Chansela wa Ujerumani, Angela Merkel

Mjini Berlin, Chansela wa Ujerumani Angela Merkel alisema “kitu kama hiki kimevuka mpaka huwezi hata kufikiria. Huu ni mzigo mkubwa sana kwa ndugu wa waathirika”.

Mwendesha mashtaka Robin alisema “hakuna kitu chochote cha kufikiria kuwa ni shambulizi la kigaidi lakini tutaona mienendo ya mtu huyo”.

Alisema rubani msaidizi ambaye ni raia wa Ujerumani aliiangusha ndege “kwa sababu ambazo hatuzijui kwa hivi sasa”.

XS
SM
MD
LG